Mbwembwe zote zile ASFC Bingwa tunapewa Sh. 50m tu?

Mbwembwe zote zile ASFC Bingwa tunapewa Sh. 50m tu?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
BAADA ya Simba kukabidhiwa kombe la ubingwa wa FA bila zawadi ya pesa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema itakabidhiwa fedha wakati wowote.

Simba imetwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Yanga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, juzi.

Baada ya ushindi huo, Simba ilikabidhiwa zawadi ya kombe bila pesa taslimu Sh50 milioni ambazo hutolewa kwa bingwa.

Jana, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema suala la zawadi ya mshindi lipo chini ya mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi au katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao.

“Lini bingwa wa FA atakabidhiwa zawadi ya pesa hilo linashughulikiwa na mkurugenzi wa mashindano na katibu wao ndiyo wana ratiba ya jambo hilo,” alisema Karia.

Madadi alipoulizwa alisema mchakato wa kukabidhi zawadi kwa bingwa utafanyika wakati wowote na Simba itakabidhiwa pesa zao.

My Take
:
Mbona Azam Tv walikuwa na mabango mengi sana. Yaani 50m kweli? Au hii ni hela ya TFF tu, kuna donge la Azam?
 
Simba wakati mwingine waangalie gharama kabla ya kushiriki mashindano, hii mechi wamepelekwa Kigoma mbali, wamekosa mapato ya uwanjani kutokana na uwanja kuingiza washabiki wachache halafu wanapewa pesa kiduchu. kwanini wanakubali kuwa wanyonge namna hiyo.
 
Nadhani wahusika wanapita humu..hata zawadi ya ligi kuu bado ndogo,ngoja tuone kwa uwekezaji wa azam may be next season mambo yakawa mazuri!
 
haiwezekani, 50m? ambayo wachezaji wa utopolo wanaenda kuzichoma zaidi ya hizo bata la morocco?
 
Back
Top Bottom