MC Alger wamemtupia virago kocha wao Patrice

MC Alger wamemtupia virago kocha wao Patrice

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Haya sasa kumekucha huko naona wapizani wa Yanga nao wamefukuza kocha.

Sasa je itakuwa faida kwa timu ya Wananchi kulamba alama 3 kwa Mkapa?
=================

Klabuni ya Mouloudia Club d’Alger almaarufu MC Alger ambao ni wapinzani wa Yanga Sc kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wamethibitisha kuachana na kocha wao Patrice Makubaliano ya pande zote mbili ikiwa ni muda mfupi kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan katika dimba la Julai 5 1962.

Beaumelle (46) raia wa Ufaransa aliiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Algeria msimu wa 2023/24 pamoja na kuipeleka kwenye fainali ya kombe la Algeria.

Ndani ya miezi 20 ya utumishi wake klabuni hapo ameiongoza klabu hiyo kushinda mechi 36, sare 19 na vipigo 10 kwenye michezo 65.

Screenshot 2024-12-16 150225.png
 
Kazi ya ukocha wa mpira ndivyo ilivyo. Maana hata Yanga walimuaga Gamondi.
 
Back
Top Bottom