Mc ashindwa kuendesha sherehe baada ya kubaini bi harusi anayeolewa ni ex wake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kisanga kilizuka katika harusi eneo la Mwatate, Taita Taveta nchini Kenya baada ya jamaa 'Mshereheshaji/MC) aliyekuwa akisimamia sherehe hiyo kushindwa kuzungumza na kulazimika kutupa Kipaza sauti (maikorofoni) alipogundua ni Mpenzi wake wa zamani (Ex wake) aliyekuwa akiolewa.

Penyenye zinasema kuwa kisura alimtoroka jamaa kwa dharau akimwambia kwamba hawezi kuolewa na mtu maskini.

Kulingana na Taifa Leo, jamaa huyo ni mwalimu na wengi walimjua sana kutokana na sauti nzuri na maneno ya kumtoa nyoka pangoni ila siku hizo alibaki amekauka mdomo.

Inasemekana kuwa kisura aliyekuwa akiolewa alikuwa mpenzi wa zamani wa barobaro huyo.

Licha ya jamaa kujibidiisha kupiga vibarua na kumfurahisha mrembo huyo, bado aliachwa kwenye mataa.

Duru zinaarifu kwamba jamaa alipogundua anaongoza harusi ya mpenzi wake wa zamani aliyempenda kwa dhati aliingiwa na huzuni mwingi akashindwa la kusema.

Penyenye zinaarifu kwamba wawili hao hawakukosana walipoachana ila mrembo alijiondoa kwa upole na kuanza uhusiano na jamaa mwingine aliyekuwa na donge nono mfukoni.

“Heri niolewe na rubani. Mwalimu kama wewe unayekisifia Kiswahili chako na sauti nzuri utanipa nini?” jamaa alikumbuka mrembo akimuuliza na hapo akaishiwa nguvu mwilini na kuangusha kipaza sauti.

Aliinama akakiokota lakini akaanza kukohoa, hata maji aliyoletewa hayakumfaa kitu.

Hatimaye lofa aliamua kukabidhi maikorofoni akiashiria kwamba hangeendelea na sherehe, huku kisura akionekana akimtazama na kutabasamu akifurahia mateso ya jamaa.

“Alinikataa aolewe na jamaa yule mwenye sura ya nyani! Jamani! Kumbe pesa ni sabuni ya roho!” jamaa alisikika akisema huku akisaidiwa kuondoka jukwaani kwani alikuwa ameisha nguvu kabisa.

Waliomsikia walimuonea huruma ila hakuna jinsi wangeweza kumsaidia.

“Mbona wanawake wanatesa majamaa hivi jamani?” jamaa mmoja alisema kwa huruma. “Lakini pia ukiachwa achika tu na ukubali,” mrembo mmoja naye alimjibu.

Semasema zinaarifu kwamba jamaa alipopata mpenyo, alitumia mlango wa nyuma kutoweka katika sherehe hiyo.
 
Walimu wataambulia kwenda peponi tu lakini wanafanana na jamii za kitaa hasa Tanzania
 
Mwenye nacho ataongezewa milele na milele, na asiye nacho atanyang'anywa hata kile alicho nacho.
 
Badala ya kushukuru amepata kazi ya kumwingizia pesa anabaki kuendekeza tamaa na wivu wa mapenzi. Haoni kuwa angeitenda kazi yake ya u Mc vema angetangaza fursa nyingine kupitia harusi ya x girlfriend wake.
 
Yuko wapi huyo MC sahi? , anafaa akatwe vibao vya maana, dadeq! 🤣 🤣 🤣
 
Kisanga kilizuka katika harusi eneo la Mwatate, Taita Taveta nchini Kenya baada ya jamaa 'Mshereheshaji/MC) aliyekuwa akisimamia sherehe hiyo kushindwa kuzungumza na kulazimika kutupa Kipaza sauti (maikorofoni) alipogundua ni Mpenzi wake wa zamani (Ex wake) aliyekuwa akiolewa.

Penyenye zinasema kuwa kisura alimtoroka jamaa kwa dharau akimwambia kwamba hawezi kuolewa na mtu maskini.

Kulingana na Taifa Leo, jamaa huyo ni mwalimu na wengi walimjua sana kutokana na sauti nzuri na maneno ya kumtoa nyoka pangoni ila siku hizo alibaki amekauka mdomo.

Inasemekana kuwa kisura aliyekuwa akiolewa alikuwa mpenzi wa zamani wa barobaro huyo.

Licha ya jamaa kujibidiisha kupiga vibarua na kumfurahisha mrembo huyo, bado aliachwa kwenye mataa.

Duru zinaarifu kwamba jamaa alipogundua anaongoza harusi ya mpenzi wake wa zamani aliyempenda kwa dhati aliingiwa na huzuni mwingi akashindwa la kusema.

Penyenye zinaarifu kwamba wawili hao hawakukosana walipoachana ila mrembo alijiondoa kwa upole na kuanza uhusiano na jamaa mwingine aliyekuwa na donge nono mfukoni.

“Heri niolewe na rubani. Mwalimu kama wewe unayekisifia Kiswahili chako na sauti nzuri utanipa nini?” jamaa alikumbuka mrembo akimuuliza na hapo akaishiwa nguvu mwilini na kuangusha kipaza sauti.

Aliinama akakiokota lakini akaanza kukohoa, hata maji aliyoletewa hayakumfaa kitu.

Hatimaye lofa aliamua kukabidhi maikorofoni akiashiria kwamba hangeendelea na sherehe, huku kisura akionekana akimtazama na kutabasamu akifurahia mateso ya jamaa.

“Alinikataa aolewe na jamaa yule mwenye sura ya nyani! Jamani! Kumbe pesa ni sabuni ya roho!” jamaa alisikika akisema huku akisaidiwa kuondoka jukwaani kwani alikuwa ameisha nguvu kabisa.

Waliomsikia walimuonea huruma ila hakuna jinsi wangeweza kumsaidia.

“Mbona wanawake wanatesa majamaa hivi jamani?” jamaa mmoja alisema kwa huruma. “Lakini pia ukiachwa achika tu na ukubali,” mrembo mmoja naye alimjibu.

Semasema zinaarifu kwamba jamaa alipopata mpenyo, alitumia mlango wa nyuma kutoweka katika sherehe hiyo.

Hivi kwanini Kenya kuna vituko sana?!
 
Maisha ya uhusiano yana mambo mengi sana,salio linatakiwa liwe linasoma vizuri,kutoana 'out', wakati huo huo uwe unapeleka ukuni kisawasawa.
 
Eti ....."Heri niolewe na rubani. Mwalimu kama wewe unayekisifia Kiswahili chako na sauti nzuri utanipa nini?”..... [emoji1] Ni kama video ni kama drama. Sio fair hata kidogo. [emoji1]
 
Kha! Yaani tu, hicho kipaza sauti ninaweza kukipasua vipande na kuondoka, hivi mbona walimfanyia huo unyama, ilikua njama au nini...
 
Back
Top Bottom