Diehard
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 470
- 356
nakumbuka huko nyuma mch. rwakatale wa mikocheni B assemblies of God aliwahi kutumia mtindo wa kununua vitambaa (leso) vyeupe na kuviombea kisha anawapa watu ati wakivitumia kama kuviwekwa kwenye viipaji vya nyuso zao au za wagonjwa wao nyumbani, wanapona maradhi yanayowasumbua. shuhuda nyingi sana zilitolewa na ilifikia mahali kama mtu yumo ndani ya basi akielekea kanisani na akagundua kuwa kasahau kitambaa nyumbani huteremka na kurudi kukifuata, yaani kikawa sacred kupita kitambaa cha kawaida.
binafsi sikuwahi kuunga mkono tabia ya huyu mama kuombea vitambaa na kuvifanya kama hirizi, na kwa kweli sikuona msingi wa jambo hilo kitheolojia.
sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.
kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!
binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!
siwezi kutoa hukumu juu ya babu lakini naamini Mungu ni mkuu na muweza kuliko anavyoonekana kupitia hali ya huko loliondo. biblia inatuasa, tusimzimishe Roho, tusitweze unabii, tujaribu mambo yote tushike lililojema na tujitenge na ubaya wa kila namna (1 thesalonike 5:19-22)
naomba mnielewe kuwa sikejeli ndugu zetu wanaogua magonjwa mbalimbali sugu wanaopata faraja ya pekee huko samunge kwa babu, la hasha. haya ni mawazo yangu tu yaliyojikita kutazama jambo zima kitheolojia zaidi na sijatumwa na mtu yoyote. pia tusiwabeze wale wanaoonyesha kuhoji mantiki ya kanisa la KKKT kujipambanua pamoja na huduma hii ya babu.
HUKUMU NI ZAKE BWANA
mbarikiwe sana wapendwa
Glory to God
Wawewza kuniambia kwanini wana waisrael walitakiwa kuimgeukia yule nyoka wa shaba aliyewekwa na musa na sio wageukie upande mwingine. waweza pia kuniambia kwanini wengine waliambiwa wakajichovye marasaba kwenye mto wenye maji machafu wa Yordani na wengine wakaambiwa imani yao imewaponya? Usijemjaribu mungu kwa imani finyu uliyonayo, na wala usije ukadhani ati neema hii itashuka israel au kwa yeyote mwenye ngozi ya rangi nyeupe na wala usijaribu kuwakatisha tamaa wengine wenyematatizo na imani ya kupata neema hii ya babu.
Mungu kamwe hawezi kuwaponya wanafiki na wenye imani haba.