Mc cane
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 5,570
- 10,517
Salam wakuu,
Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu ambapo kutakuwa na Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na kila Chama kinatazamiwa kusimamisha mgombea/wagombea katika nafasi hizo za uongozi.
Nimeona niongelee mchakato huu ndani ya CHADEMA kwa kuwa mara baada ya Freeman Mbowe kutangaza nia ya kugombea Urais kumekuwa na mtazamo tofauti kutoka kwa Watanzania.
Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakimlaumu Mbowe kwa kitendo cha kuamua kugombea, wako walioamini kwamba kwa kufanya hivyo amevuruga/atavuruga mshikamano ndani ya Chama wakati wa kumsaka na/au baada ya mchakato wa kumpata mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama chao.
Baadhi wamepongeza hatua hiyo wakiamini Mbowe ameamua kugombea kwa kuwa hiyo ni haki yake ya kidemokrasia kusimama kukiwakilisha Chama katika nafasi hiyo kubwa kabisa nchini.
My Verdict
Kushambuliwa kwa Mbowe hivi karibuni, hali ya Mbowe kule jimboni (hii ni pamoja influence ya ya Serikali kwenye hili) vimechochea maamuzi yake kuamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais
Kuna watu ndani ya chama/wapenzi wa chama waliamini kuwa hii nafasi ya kuwakilisha Chama ni ya Tundu Lisu, kuingia kwa Mbowe kwenye equation kutaleta mtazamo na matokeo tofauti kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa Urais na Pengine kwenye siasa za chama kwa siku zijazo. Pengine hapa, Lazaro Nyalandu na Peter Msigwa wameongezewa nafasi za kufanikiwa katika mbio zao kwani hali halisi inaonesha kuwa wapiga kura wa Mbowe ndio wapiga kura wa Lisu.
Mpango/Mchezo wa CHADEMA kwenye Uchaguzi mkuu huu wa mwaka huu 2020. Sote tunafahamu kuwa kumekuwa na propaganda/maneno ya hapa na pale kuhusu kutokuwepo na demokrasia ndani ya CHADEMA hususani inapotokea Mbowe anagombea nafasi flani ndani ya Chama. Kwa Mbowe kuamua kugombea akishindwa kwa kiasi kikubwa zile propaganda/maneno ya kuwa Mbowe ni CHADEMA au CHADEMA ni Mbowe zitakuwa, zitahitaji mtu awe chizi ili aendeleze maneno hayo. Mbowe AKISHINDA kwenye Uchaguzi ambao Lisu anagombea na kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA bado watu watakubali kuwa Mbowe ameshinda kihalali kwani kama hajashinda kihalali Lisu si mtu wa kukaa kimya inapotokea rafu imefanyika katika jambo lolote.
Mwisho mimi ningekuwa nipo CHADEMA ningefurahi ndugu Mbowe kuingia kwenye mchakato huu kwani hii ni hatua kubwa ya kuwaziba midomo wale wote waliokuwa wanasema CHADEMA hakuna demokrasia kwani kuponda wagombea wengi wanapojitokeza ni hatua ya kudhihirisha kuwa CHADEMA hakutakuwa na mchakato wa kidemokrasia.
Ningekuwa nipo upande wa CCM ningekuwa nina mashaka, ningejiuliza nini CHADEMA wanapanga. Lakini pia ningeweza kuwa na imani kuwa kitendo cha Lisu na Mbowe kugombea nafasi moja hususani ya Urais inaweza kuleta mpasuko mkubwa ndani ya Chama cha CHADEMA kwa nyakati hizi za Uchaguzi Mkuu au hata baada ya hapo
Waingereza wanasema let's wait and see