Manyenye JR
New Member
- Jul 30, 2022
- 1
- 0
Bajeti ya taifa ni mpango unaoonyesha namna serikali itakavyo kusanya na kutumia fedha kutoka vyanzo mbalimbali. Hii inaelezea namna fedha zitakavyo kusanywa kutoka vyanzo mbalimbali na namna zitakavyotumika kutokana na vipaumbele vya taifa.
Mchakato wa bajeti katika mamlaka za serikali za mitaa inahusisha hatua nne ambazo ni
Uundaji wa bajeti
Kujadili na kupitisha bajeti
Utekelezaji wa bajeti na
Usimamizi na ufuatiliaji wa bajeti
Uundaji wa bajeti, kazi inaanza kwa serikali za vijiji au mitaa kupitia vipaupmbele katika maeneo yao na kupanga mipango namna watavyopata fedha na kutekeleza hiyo mipango kwa kuzingatia mapato ya ndani na nje ya kijiji au mtaa. Kwa hiyo vyombo vya uundaji wa bajeti katika mamlaka za serikali za mitaa ni serikali za vijiji na mitaa.
Kujadili na kupitisha bajeti, baada ya bajeti kuandaliwa katika serikali vya vijiji na mitaa zinatakiwa kuwasilishwa katika mkutano wa adhara wa kijiji au mtaa kwa mjini kwa ajili ya kujadiliwa na kupishwa na baada ya mkutano wa hadhara kupitisha inatakiwa ifikishwe katika kamati ya maendeleo ya kata kwa kujadiliwa na kupishwa na hatimaye kuwasilishwa halmashauri kwa ajili ya kujadiliwa katika baraza la madiwani.
Utekelezaji wa bajeti, hii inahusisha ukusanyaji wa mapato na utowaji wa huduma pamoja na utekelezaji wa miradi, utoaji wa repoti na kutoa taarifa ya mapato na matumizi katika maeneo mbalimbali ya halmashauri kwa kupitia mbao za matangazo na mikutano ya hadhara.
Usimamizi na ufuatiliaji, njia ambazo huwa zinatumika katika ufuatiliaji ni kutoa repoti za mda mfupi, ukaguzi wa ndani na nje, utekelezaji wa miradi, ubora wa miradi na kupitia taarifa za mapato na matumizi katika maeneo yote ambapo fedha zimetumika ili kubaini kama kuna usawa kati ya mapato na matumizi. Mchakato huu wote wa bajeti kwenye mamlaka ya serikali za mitaa unafanyika chini ya sheria ya serikali ya mitaa 1982 na mabadiliko yake.
Hali ya ushiriki wa vijana katika mchakato wa bajeti
Ushiriki wa vijana katika mchakato wa bajeti ya taifa sio wa kuridhisha hali inayosababisha mipango mingi kutohusisha vijana kwa kushidwa kugusa masilahi yao kwa upana, sababu zanazopelekea ushiriki mdogo ni pamoja na kutokuwepo kwa majukwaa huru kwa vijana ya kujadili bajeti kuanzia hatua ya uanzishwaji hadi hatua ta usimamizi na tadhimini maana njia kuu inayotumika ni mikutano ya hadhara ambayo inauganisha na wazazi wa vijana kwa hiyo inakuwa ngumu kwa vijana kuwa huru kwa kutoa mawazo yao kuhusu bajeti jadili wa.
Nini kitatokea kama vijana watashiriki ipasavyo
Kutaongeza uwazi wa bajeti na miradi ya maendeleo, kama vijana watashiriki kuanzia mwanzo wa uanzishwaji wa bajeti mpaka utekelezaji wake kutafanya wao kujua kila kinachoendelea kuanzia kwenye bajeti yenyewe mpaka miradi inayotekelezwa kwa kutumia bajeti hiyo.
Kuzuia vitendo vya rushwa kwa sababu vijana watashiriki kila hatua kwa kuangalia upitishwaji wa bajeti, utumiaji wa bajeti na kuhakikisha ubora wa miradi inayotekelezwa kupitia bajeti iliyoandaliwa bila fedha nyingine kutumika nje ya malengo yaliyokusudiwa.
Kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha za umma, ushiriki wa vijana utachochea ubainifu sahihi wa maitaji na uelekezi wa fedha katika maitaji yaliyo sahihi kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa kwa mda wote wa upangaji na utekelezaji wa bajeti Husika.
Kuhakikisha maitaji ya vijana yanaingizwa katika mipango na kupangiwa bajeti kwa ajili ya utekelezaji na kusababisha kuondoka kwa baadhi ya changamoto zinazowakumba vijana kama ukosefu wa ajira maana wataweza kutimiziwa maitaji yao na wao kufanya shighuli za kuwaingizia kipato.
Mbinu zinazoweza kuongeza ushiriki wa vijana katika mchako wa bajeti
Kuazishwa kwa kamati za bajeti za vijana katika ngazi ya vijiji, mitaa na kata, ambapo hizi kamati zitakuwa majukwa huru ya vijana kukutana na kujadili vipaumbele vyao bila uwepo wa wazazi wao. Kamati hizi ziwe zinakaa kabla ya serikali ya kijiji au mtaa kukaa ili vijana wawasilishe vipaumbe vyao kwa kujadiliwa na serikali ya kijiji au mtaa na atimaye mkutano mkuu wa bajeti wa kijiji au mtaa.
Kutumia mitandao ya kijamii, Radio na TV kama njia ya vijana kuwapa taarifa na kujadili bajeti, mfano wattsap, kukiwa na group la vijana kwenye mtaa na likawa maalumu kwa kujadili mambo ya bajeti itakuwa rahisi wao kushiriki mara kwa mara, lakini pia halmashauri zinaweza kufungua akaunti za vijiji na mitaa kwenye club house na facebook ili vijana wawe wakutana huko kila baada ya miezi mitatu wanajadili vipaumbele vyao na kuviwasilisha serikalini kwa wakati, kuanzisha vipindi vya redio na TV kuhusu mchakato wa bajeti ya taifa ili kuwapa uelewa vijana.
Kila kijiji na mtaa kundaa mkutano wa mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu, ili kuruhusu vijana kujadili taarifa ya mapato na matumizi kupitia kamati zao na kupeleka ufafanusi wa kundi la vijana katika mkutano wa hadhara.
Kuendelea kutumia mfumo wa fursa na vikwazo katika maendeleo (O&OD), opportunity and obstacle to development ambao hutoa fursa kwa watu wengi kushiriki katika mchakato wa kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kuendelea kuajili vijana katika nafasi za maafisa watendaji wa vijiji, mitaa na kata ili kuruhusu vijana waliopo katika mitaa, vijiji na kata kupata ushirikiano kwa urahisi kutoka kwa vijana wenzao ambao ni viongozi katika maeneo hayo
Naomba kuwasilisha.

Upvote
1