Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
Ulipoharibiwa mchakato wa katiba mpya na kikwete, niliandika yafuatayo:
Kheri tungekuwa na kundi moja la bunge maalum la katiba. Kheri tungekuwa na Tanzania kwanza, makundi ya CCM na UKAWA (upinzani) yangefutwa, tubaki na bunge maalum la katiba lenye wajumbe wa tanzania kwanza.
Kheri tungekuwa na Rais asiyekuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa angezindua bunge maalum la katiba ya Tanzania kwanza, na si msimamo wa chama chake CCM. Kheri tungekuwa na wajumbe jasiri wa bunge maalum la katiba tungekuwa na kura ya wazi.
Kheri tungewaheshimu wajumbe waoga tungekuwa na kura ya siri, ili wakiwa sirini wapige kura zisizosuta dhamira ya nafsi zao.
Kheri tungeiweka wazi tanganyika tusingejificha kwenye muungano au kujigeuza kimakosa kuwa tanzania bara wakati zanzibar haikuwahi kuungana na tanzania bara, bali tanganyika. Ikumbukwe kuwa hatujawahi kuwa na nchi iitwayo tanzania bara. Kwenye hati ya muungano haimo! Kheri tungeijua historia ya zanzibar vizuri jinsi ilivyotukuka kimataifa kwa karne nyingi, tusingeificha kwenye muungano.
Je, lini zanzibar itakuja kuwa dubai (UAE) ya Afrika kama ilivyowahi kuwa Kuba (Cuba) ya afrika!? Na je, tutaishuhudia kizazi chetu au tutaacha wanetu waje kutulaani? Na je, vipi tanganyika yenye utajiri wa kila sampuli na kuweza kuwa nchi itoayo misaada - donor country!?
Sent using jamii forums mobile app