Mchakato wa Katiba Mpya upo njiani kutekelezwa

Mchakato wa Katiba Mpya upo njiani kutekelezwa

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu alisema atashughulikia suala la Katiba Mpya na kuna watu wengine wanahoji kwanini mchakato wa Katiba Mpya unachelewa.

Sababu za kuchelewesha Katiba Mpya Rais Samia Suluhu anataka kila mwananchi ashiriki kikamilifu katika mchakato wa kuleta Katiba mpya kwasababu Katiba ni ya nchi na mwananchi hivyo kila mtu ana uhuru wa kushiriki na itachukua muda ili kukamilisha
 
Mwanzoni alisema katiba mpya isubiri ajenge uchumi.

So far inaelekea anaharibu uchumi badala ya kuujenga.

Tangu aingie madarakani hali ya uchumi imekuwa mbaya zaidi, kuna mfumuko wa bei, bidhaa adimu hazishikiki, na matozo yameongezeka.

Kwa msingi huo suala la kujenga uchumi kabla ya kuanza katiba mpya ama ilikuwa ni uongo, au haliwezekani.

Mchakato wa katiba mpya, na kusimikwa kwa mifumo ya kidemokrasia inayotoa haki sawa kwa vyama vyote, uanze sasa hivi bila kuchelewa.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Tunataka KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi itakayoweza kumtoa sa100 na CCM madarakani.
 
Katiba mpya ni sasa.
Katiba ya sasa imezalisha wabunge wanaogonga meza na kusifu tu
Katiba ya sasa imezalisha majaji wa michongo na kesi za michongo
Katiba ya sasa imezalisha wizi kupitia TOZO.
Katiba ya sasa RAIS ni mfalme hakuna wa kumhoji.
Katiba ya sasa imetuletea wabunge hewa.
Katiba ya sasa imezalisha muungano hewa.
Katiba ya sasa Mawaziri wanatukana wananchi.
Katiba ya sasa tukihoji tunaambiwa tuhamie BURUNDI kwanini si Japan au Germany ?.
Katiba ya sasa Rais KODI zetu hazijulikani matumizi yake,majenzi ya barabara,madaraja,madarasa,matundu ya choo ni fedha za RAIS na akizitoa ni hisani yake tunapaswa kumshukuru na kumwabudu.
Katiba ya sasa Rais anateua kuanzia JANUARY hadi JANUARY ni mwendo wa kuteua tu.
Katiba ya sasa Police wanaua RAIA halafu wanajifu wameua PANYA ROAD.
Katiba ya sasa hakuna kuhoji uteuzi wa Rais,fikiria ACP Kingai hajui hata PGO leo ni DCI.
Katiba ya sasa ni majanga kwa kizazi kijacho.
 
Rais Samia Suluhu alisema atashughurikia suala la katiba mpya na kuna watu wengine wanahoji kwanini mchakato wa katiba mpya unachelewa.

Sababu za kuchelewesha katiba mpya Rais Samia Suluhu anataka kila mwananchi ashiriki kikamilifu katika mchakato wa kuleta katiba mpya kwasababu katiba ni ya nchi na mwananchi hivyo kila mtu anauhuru wa kushiliki na itachukua muda ili kukamilisha
RASMU ya WARIOBA iliwapitia Wananchi wote
 
Mwanzoni alisema katiba mpya isubiri ajenge uchumi.

So far inaelekea anaharibu uchumi badala ya kuujenga...
Rais Samia Suluhu yeye sio chanzo cha mfumko wa bei chanzo ni vita vya ukraine lakini amepambana kupunguza gharama za maisha kwa kutoa bil 100 kila kmwezi kwaajili ya mafuta pia katiba mpya si kukurupuka ni kujipanga na inatakiwa wananchi watoe mawazo yao kuusu katiba mpya kwaiyo katiba mpya ni mchakato wa muda mrefu
 
Tunataka KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi itakayoweza kumtoa sa100 na CCM madarakani.
Katiba ni process mzee kwaiyo itachua muda then huu utawala sio ule tuliuzoea wa kutumia nguvu huu serikali ya sasa inasikiliza wananchi na kufanyia kazi kwaiyo uchaguzi ujao utakua fair kabisa lakini nikuhakikishie Rais Samia atashinda kwa asilimia zaidi ya 80
 
Rais Samia Suluhu yeye sio chanzo cha mfumko wa bei chanzo ni vita vya ukraine lakini amepambana kupunguza gharama za maisha kwa kutoa bil 100 kila kmwezi kwaajili ya mafuta pia katiba mpya si kukurupuka ni kujipanga na inatakiwa wananchi watoe mawazo yao kuusu katiba mpya kwaiyo katiba mpya ni mchakato wa muda mrefu
Raisi anatakiwa kutatua matatizo yote yanayotukabili hapa nchini.

Hii habari ya kudai matatizo fulani hayamhusu ni jitihada za kulea uvuvi na kutokuwajibika.

Raisi alipwa vizuri, anatunzwa na kulishwa, analindwa kuliko raia yoyote yule hapa nchini.

Haiyumkiniki wananchi wanapatwa na changamoto aache kuzitatua kwa visingizio kuwa changamoto hizo zimesababishwa na matatizo ya nje.

Kuhusu katiba mpya sio kweli kwamba tumekurupuka. Suala la katiba mpya lilishughulikiwa kwa kina na Tume ya Mzee Warioba.

Kwa bahati mbaya Samia Suluhu Hassan akiwa makamu mwenyekiti wa bunge pamoja na manazi wenzake wa Ccm walivuruga mchakato wa katiba.

..Ssh anajua ni jinsi gani walikwamisha upatikanaji wa Katiba mpya, sasa ni wajibu wake kuukwamua bila kutupotezea muda.
 
Atashinda njaa labda.😀😀😀

Alikuwa Makamo mkt Bunge la Katiba.

Kwamba ameshajitoa UFAHAMU kuwa Tume Ile ilipita Nchi nzima kukusanya maoni?
Katiba ni process mzee kwaiyo itachua muda then huu utawala sio ule tuliuzoea wa kutumia nguvu huu serikali ya sasa inasikiliza wananchi na kufanyia kazi kwaiyo uchaguzi ujao utakua fair kabisa lakini nikuhakikishie Rais Samia atashinda kwa asilimia zaidi ya 80
 
Rais Samia Suluhu alisema atashughurikia suala la katiba mpya na kuna watu wengine wanahoji kwanini mchakato wa katiba mpya unachelewa.

Sababu za kuchelewesha katiba mpya Rais Samia Suluhu anataka kila mwananchi ashiriki kikamilifu katika mchakato wa kuleta katiba mpya kwasababu katiba ni ya nchi na mwananchi hivyo kila mtu anauhuru wa kushiliki na itachukua muda ili kukamilisha
Kwahiyo yale maoni yaliyokusanywa na mzee warioba na tume yake yalikuwa sio ya wananchi ila mafisi porini?

Hebu acheni uzwazwa we jamaa. Na laiti ccm na mama Samia mngejua mngeleta katiba mpya sasa ili angalau mko madarakani mnaweza kujaribu-jaribu kujiwekea mazingira ya kujipendelea maana kwa jinsi mnazidi kuchelewa hili fukuto la katiba mpya ni bomu, aminini nawaambia msisubiri lilipuke lenyewe, mtajikuta hamna namna hata ya kuchagua wajumbe wa kuleta hiyo katiba mpya. Mngejua mngetumia ule msemo wa ukila na kipofu usimshike mkono ili umpige kwa kula nyama nying japo pia haitasaidia saaaaaana.

Trust my words we jamaa, KATIBA MPYA ITAKUJA TANZANIA NA CCM ISIPOANGALIA NA KUCHEZA KARATA ZAKE VIZURI ITAKUWA CHAMA CHA UPINZANI. Ni suala la muda tu.
 
Ni nchi ipi kwa sasa haina mfumko wa bei hapa dunia?.

..Sina haja ya kujua kwasababu hainihusu.

..Kwani ni dhambi Tanzania kuwa nchi mojawapo, au hata pekee, isiyokuwa na mfumuko wa bei?

..Raisi na Waziri wa fedha wanafanya kazi gani?

..Je, bado wanaendelea kupokea mshahara?
 
Katiba bora ili tuipate ni lazima TUCHAPANE kwanza. Vinginevyo tusahau.
 
Kama mnasubiri kuipata KATIBA MPYA wakati wa utawala huu wa Mhe.Dk. SAMIA SULUHU HASSAN,...hamtaipata ng'odo!!!

Mkiipata mniite mbwa nimekaa paleeee!!!

Hivi nyie mnafikiri KATIBA MPYA ni suala la mchezomchezo eeh? Aaaasubutu!!!!
 
Back
Top Bottom