SoC04 Mchakato wa kitaifa ufanyike kuitengeneza Tanzania tuitakayo

SoC04 Mchakato wa kitaifa ufanyike kuitengeneza Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 17, 2024
Posts
7
Reaction score
5
Mabadiliko yoyote ili yatokee ni lazima kuwe na mchakato maalumu wa kuleta hayo mabadiliko. Taifa ili kujikwamua kutoka hali duni kuwa taifa linaloendelea au lililopiga hatua katika nyanja mbalimbali lazima ufanyike mchakato wa maalumu wa kuleta mabadiliko yanayotakiwa.
Viongozi na raia mijini na vijijini washiriki kuandaa na kutekeleza maono ya taifa. Mbinu hizi hapa chini zinaweza kutumika kuibadilisha Tanzania.

A) Mchakato wa kukusanya maoni ufanyike kwa taifa zima kupata mapendekezo ya taifa tulitakalo.
Mchakato unaotumika katika kutunga katiba unaweza kutumika katika mchakato wa mabadiliko ya Tanzania. Serikali iandae watu watakao zunguka nchi nzima kuandika maoni mbalimbali ya watu juu ya taifa tulitakalo. Wananchi wote washiriki kikamilifu kwani hata katika mabadiliko yatakayopendekezwa watapaswa kuyaishi kulingana na makubaliano.

B) Kuchambuliwa na kuhaririwa kwa maoni na mapendekezo yaliyokusanywa juu ya Tanzania tuitakayo.
Baada ya kukusanya maoni sasa ni muda mwafaka wa kuyahariri na kuyachambua. Wawakilishi au wataalamu wanaweza kutumiwa kushughulikia uchambuzi huo. Umakini wenye tija utumike ili kupata malengo yatakayofikiwa kwa muda utakaowekwa.

C) Maoni na mapendekezo yaliyopatikana yawe ndio malengo na maono ya Tanzania tuitakayo,hivyo yawekwe wazi kwa taifa zima ili kila mtu ajue tulipo na tunapotaka kwenda.
Malengo na maono hayo yawekwe kwenye maandishi kwaajili ya utekelezaji wa vitendo. Ikiwezekana kila mtu awe na nakala ambayo itatumika kama dira ya taifa. Shughuli za kila siku ziakisi kuleta mabadiliko kulingana na makubaliano yaliyowekwa.

D) Muda uainishwe wa kutimiza malengo na maono ili kuyaendea mabadiliko.
Katika utekelezaji wa malengo na maono muda ndio kipimo cha kufikiwa au kusuasua. Muda uliowekwa uheshimiwe kwani ukishapita huwa haurudi. Uwajibikaji uwe kipaumbele kwa viongozi na wananchi ili kwenda sawa na muda wa malengo yaliyowekwa.

E) Vitafutwe vipaumbele vya kutekeleza haraka zaidi.
Katika malengo na maono yoyote huwa kunakuwa na vipaumbele vya kutimiza haraka zaidi. Haya huwa ni malengo ya muda mfupi yanayofikiwa kila siku.Nguvu kubwa iwekezwe katika kuyafanya kwa kufokasi sana ili kutokutoka nje ya malengo yaliyokusudiwa.

F) Sheria zitungwe kusimamia utekelezaji wa malengo na maono.
Ili taifa lisonge lazima kuwe na sheria zitakazosimamia utekelezaji wa maono hayo. Ukiukwaji wa sheria hizo unaweza kuzolotesha mabadiliko yaliyokusudiwa. Hivyo viongozi na raia wafuate sheria hizo ili kufikia matokeo yaliyokusudiwa.

G) Viongozi na wananchi washirikiane kukamilisha malengo na maono.
Nguvu kubwa ya viongozi na wananchi iwe kuleta matokeo chanya. Ushirikiano wa viongozi na raia utawezesha mawasiliano na kuwa na taarifa sahihi na kuongeza uchapakazi. Kuwe na usawa katika utekelezaji wa majukumu na usimamiaji.

H) Tathmini ifanyike kila baada ya muda fulani ili kuona mafanikio na mapungufu.
Katika mchakato wowote wenye malengo ni lazima kuwe na tathmini ya kuona malengo na maono yaliyofikiwa au kutofikiwa. Hii itarahisisha kuboresha mbinu za utekelezaji wa malengo hayo na katika mapungufu kuongeza bidii zaidi. Tathmini inaweza kuleta picha kama tunasonga mbele au la. Tathmini inaweza kufanyika kila siku, mwezi , mwaka au miaka kadhaa.

Kwa nyongeza, Tanzania tuitakayo katika miaka 5-25 ni malengo ya muda mrefu. Ili kufikiwa ni lazima kuwe na malengo ya muda mfupi yatakayotekelezwa kila siku ili kuyafikia yale ya muda mrefu. Mipango na mikakati ya utekelezaji iwekwe ili kurahisisha mchakato wa kufikia hatima iliyokusudiwa.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom