Mchakato wa kununua nyumba

Mchakato wa kununua nyumba

faru john junior

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2016
Posts
1,596
Reaction score
1,719
Wanajanzi habari za asubuhi. Ni matumain yangu kuwa wote mko salama kwa wale wagonjwa nawapa pole sana na mwenyezi Mungu atawaponya,sambamba na kauli tata za waziri jafo tuwe wavumilivu.

Naomba niende kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kuna nyumba inauzwa mkoa wa Mwanza sasa bei kama iko ndani ya uwezo wangu,ningeomba wazoefu wa haya mambo ya kununua na kuuza je mambo gani ya msingi kujua ili usitapeliwa katka biashara za aina hii binafsi nyumba nimetumiwa tu picha ila physically sijaiona na alinitumia hyo picha ni dalali.

Sasa kuepuka mambo ya kwenda mahakaman kwa biashara kutokwenda vzri ni lazima mtu uwe makini kuepuka usumbufu wa aina yoyote.

Naomben ushauri wenu kwani ni bora nikawa proactive kuliko kuwa reactivate

Asante sana
 
Ndugu nakushauri nenda kaione hiyo nyumba haraka kabla ya hela. Baada ya kuikagua na kuona na dalali, panga siku uende ukiwa peke yako au na mkeo mkaongee majirani wawape historia ya hiyo nyumba (dalali asijue). Pia ulizia kama kuna mgogoro wa kifamilia. Ukiridhika na majibu yote hayo.

Fanyeni malipo kwa mashahidi, pia upewe valid docs kama hati ya makabidhiano n.k. Waweza hata kumtafuta mmiliki halali aseme kwanini anaiuza. Jiridhishe kwa 100%, ukiridhika.
Mungu akutangulie katika hili. Siku njema
 
Nimeongeza jambo asante sana

Ndugu nakushauri nenda kaione hiyo nyumba haraka kabla ya hela. Baada ya kuikagua na kuona na dalali, panga siku uende ukiwa peke yako au na mkeo mkaongee majirani wawape historia ya hiyo nyumba (dalali asijue).

Pia ulizia kama kuna mgogoro wa kifamilia. Ukiridhika na majibu yote hayo. Fanyeni malipo kwa mashahidi, pia upewe valid docs kama hati ya makabidhiano n.k. Waweza hata kumtafuta mmiliki halali aseme kwanini anaiuza. Jiridhishe kwa 100%, ukiridhika.
Mungu akutangulie katika hili. Siku njema
 
Wanajanzi habari za asubuhi. Ni matumain yangu kuwa wote mko salama kwa wale wagonjwa nawapa pole sana na mwenyezi Mungu atawaponya,sambamba na kauli tata za waziri jafo tuwe wavumilivu

Naomba niende kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kuna nyumba inauzwa mkoa wa mwanza sasa bei kama iko ndani ya uwezo wangu,ningeomba wazoefu wa haya mambo ya kununua na kuuza je mambo gani ya msingi kujua ili usitapeliwa katka biashara za aina hii binafsi nyumba nimetumiwa tu picha ila physically sijaiona na alinitumia hyo picha ni dalali

Sasa kuepuka mambo ya kwenda mahakaman kwa biashara kutokwenda vzri ni lazima mtu uwe makini kuepuka usumbufu wa aina yoyote.

Naomben ushauri wenu kwani ni bora nikawa proactive kuliko kuwa reactivate

Asante sana
Lingne kachukue cordinates za kiwanja cha iyo nyumba nenda halmashauri usika wataingiza cordinates hlf watakwambia kuwa icho kiwanja ni cha makazia, soko au open space isije kuwa wanauza sababu ni open space garama haizidi 50,000 kuangaliziwa watu wengi huwa wanakosea hapa
 
Back
Top Bottom