Mchakato wa Satelaiti yetu unaendelea, ukikamilika itasaidia kuboresha huduma za mawasiliano nchini hadi vijijini

Mchakato wa Satelaiti yetu unaendelea, ukikamilika itasaidia kuboresha huduma za mawasiliano nchini hadi vijijini

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ndugu Nape Nnauye, akizungumzia mafanikio ya safari ya ujumbe wa Rais Samia nchini Korea Kusini amesema kuwa...

Wenzetu wamepiga hatua kubwa kwenye miundombinu ya mawasiliano, hapa kwetu tunaendelea na uwekezaji, uwekezaji huo ni gharama, kingine wenzetu wanazalisha smart device kwa maana ya simu janja n.k, sisi kwetu tuna changamoto ya kusambaa kwa vifaa hivyo kwasababu ni ghali, moja ya eneo ambalo tumezungumza kwa kina ni kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana nao tukazalisha hapa kwetu kwa maana ya kuviunganisha vifaa ambavyo vitakuwa kwa bei nafuu ili Watanzania waweze kuvimudu

Najua swali kubwa hapa ni kwamba miundombinu vijijini ikoje, mtakumbuka bajeti yetu iliyopita tumetangaza mchakato wa kuwa na satelaiti yetu kama Nchi, mchakato huo unaendelea vizuri, zipo Timu zimeenda Duniani, Katibu Mkuu na Timu yake walikuwa China, wengine wataenda Marekani na kwingine , baada ya pale pamoja na miundombinu mingine ambayo tunaendelea lakini hili la kuwa na satelaiti yetu kama Nchi linaendelea vizuri na changamoto hizi zitapungua

Lazima tujenge utamaduni aa kufanya kazi huu utamaduni wa Watu wanashinda mtandaoni masaa 24 halafu baada ya pale mfukoni hamna kitu huu utamaduni lazima tuupige vita vinginevyo hatuwezi kutoka, na ni kupitia kazi, Watu wasifikiri kuna Mjomba atakuja mahali akuletee maendeleo ya maisha yako
 
Mnapenda kuibiwa tu, matumizi ya satelitę kwenye communication duniani ni 1% na gharama zake zipo juu.

Ampendi kutumia muda kujifunza mambo hata kwenye hii dunia ya information za bure, mnaishia kuchezea hela na kuibiwa kirahisi sana.
 
Mbongo akikutajia maneno kwamba mchakato unaendelea, kimbia sana na ikiwezekana tafuta ulinzi maalum wa jeshi.
 
Hii habari inanikumbusha maneno tuliyokuwa tunapewa enzi za kutaka kuchimba gesi Mtwara.

Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Back
Top Bottom