Mchakato wa tuzo ya Mfungaji Bora Ligi ya Tanzania hauna tofauti na mchakato wa kumpata Papa mpya huko Vatcan.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Upo umuhimu mkubwa sana TFF na Bodi ya ligi kuu Tanzania kuingia watu wa mpira (watu wenye weledi/kujua mpira) siyo wachumia tumbo.

Suala la Fistoni kalala Mayele na Saidoo Ntibazonkiza limeleta ugumu mkubwa kwa BOdi ya ligi Tanzania kufanya Nani anastahili kiatu/tuzo hiyo kwa kua tu ni wachezaji wanaotoka kariakoo na ndiyo maana Bodi ya ligi wamejifungia ndani na hawajatoa/hawajazungumza Nani anastahili kiatu kwa kuhofia lawama/kelele za mashabiki.

Laiti Kama Fistoni kalala Mayele/Saidoo Ntibazonkiza angefungana magoli na Sixtus Isabilo Bodi ya ligi wangeweka wazi mapema sana Ila kwa kua wachezaji wote wametoka kwenye timu kubwa za kariakoo (Simba na Yanga) mpaka Sasa Bodi ya ligi wanapepesa macho.

Huu mchakato wakujifungia ndani na kuchakata Nani mshindi hauna tofauti na kutafuta Papa mpya huko Vatican.

Ndani yao humo humo Kuna wanaosema apewe Saidoo wengine Fiston kalala Mayele hiyo ni kutokana na kanuni za hapa haipo Sasa kinachotumika ni Kufumba macho nakutumia mahaba tu dhidi ya mchezaji gani anapendwa sana.

Nawasilisha hoja.
 
Mpaka moshi mweupe utoke ndo anapatikana mfungaji bora
 
Unaweza Kuta hawana hata kanuni ya kuamua bingwa wa ligi endapo timu mbili zitafanana kila kitu. Wao wanasubiri itokee ndio watunge kanuni..
 
Kutoka kwa mtu wa ndani wa TFF...Wanahangaikia kupata kiatu kingine na wte watapata
 
Ndiyo kusema umekosa kabisa mifano mingine, mpaka uchague huu mfano wa kuchaguliwa kwa Papa Vatican na hizi siasa za ufungaji bora!!
Hakuna shida Ila shida unataka kuileta wewe Soma Mara mbili upate kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…