Mchakato wa Uchukuaji fomu CCM za umeya Morogoro Waanza

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
​

Mchakato wa kuchukua fomu za kuwania Umeya na Unaibu Meya wa Manispaa ya Morogoro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) umeanza rasmi leo, ambapo wanachama mbalimbali wakiwamo viongozi wa kada na watumishi wa umma wamejitokeza kuchukua fomu.

Miongoni mwa waliojitokeza ni Mwandishi wa habari Latifa Ganzeli ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum ambaye amechukua fomu kuwania nafasi ya Unaibu Meya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Morogoro Mjini, Khalid Hossein King, amesema mchakato huo utakamilika Novemba 21, 2025 saa 10 jioni, huku akibainisha kuwa muitikio wa wanachama ni mkubwa na unadhihirisha hamasa ya kushiriki uongozi wa Serikali za Mitaa.

Kwa upande wake, Bi. Ganzeli alisema uamuzi wake unatokana na uzoefu wa miaka 10 ndani ya Baraza la Madiwani na kwamba akipewa ridhaa ataweka nguvu kubwa kwenye kuongeza vyanzo vipya vya mapato, uboreshaji wa huduma za jamii na ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…