Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mkurugenzi wa Shirika la Bridge for Change, Ocheki Msuva ambaye ni mtaalamu wa siasa na utawala anayejihusisha na masuala ya vijana katika eneo la ushiriki na ushirikishwaji amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa umeisha, hivyo ni muhimu kujikita katika mazungumzo na majadiliano yenye kujenga umoja wa kitaifa kwa maslahi ya maendeleo ya taifa.
Msuva ametoa wito huo leo jijini Dodoma, ikiwa ni siku ya nne mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kutangaza matokeo ya jumla ya uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Aidha. Msuva amesema ni wakati muafaka wa kuwa na majukwaa ya mazungumzo na majadiliano yenye kujenga jamii moja ili kutoa fursa ya kuwasikiliza wale ambao wanaona kwa namna moja au nyingine hawakulizika na mchakato wa uchaguzi, na fursa hiyo itakuwa ni sehemu ya kufanya maboresho kwa mustakabali wa uchaguzi ujao.
Jambo TV