Mchanga wa kutengeneza maabara

Mchanga wa kutengeneza maabara

The Tai

Member
Joined
Dec 9, 2019
Posts
6
Reaction score
15
JE INAWEZEKANA?

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaoishi maisha ya upweke kwa muda mrefu hivyo starehe yangu kubwa baada ya shughuli zangu za kila siku ama ninapopata nafasi ya kumpumzika ni kusoma vitabu.

Hata kabla ya kuandika ninachotaka kuandika siku ya leo mapajani mwangu nilikuwa nimeshika kitabu cha UJASUSI cha muabudu mizimu bwana Yericko Nyerere.

Huko nyuma niliwahi kusoma kitabu kinaitwa ZAWADI YA ADHABU,katika kitabu hicho mwandishi alisema kwamba "hakuna kitu kisichowezekana kufanyika vile tu kufikiria jambo tu inaonesha dhahiri kwamba linaweza kufanyika".

Kwa upande mwingine katika kitabu cha ZERO TO ONE mwandishi anasisitiza kwamba hapa duniani hakuna kitu ambacho binadamu akikihitaji atakikosa ikiwa akakiwekea juhudi.

Kwa kauli mbili za waandishi hapo juu ni dhahiri kwamba sisi kama binadamu tunauwezo wa kufanya jambo lolote ikiwa tutakuwa na nia ya dhati pamoja na juhudi na hizo kauli ndizo zimenipelekea mimi kuandika haya.

Nchi nyingi duniani ikiwepo nchi yetu Tanzania hutumia mchanga katika shughuli zote za ujenzi na mchanga huo hupatikana kwa kuchimbwa ardhini hasa mitoni na makorongoni.

Kila kukicha matumizi ya mchanga yamekuwa yakiongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu majengo yanayojengwa maeneo mbalimbali.

Kwa mtu anayeona mbali ni dhahiri kabisa uchimbaji huu wa mchanga utapelekea uharibifu mkubwa wa mazingira ambao madhara yake yataonekana zaidi katika kizazi kijacho.

Sasa nilikuwa najiuliza je kama nchi tunawezaje kuzuia madhara ya uchimbaji wa mchanga ndipo nikapata wazo la kutengeneza mchanga maalumu kwa ajili ya ujenzi ambao utatengenezwa maabara.

Binafsi mimi sijasoma masuala ya Civil Engineering wala masuala ya chemical processing hivyo nimeshindwa kujibu hilo swala mpaka sasa.

Eti wataalamu wa hayo masuala je inawezekana?

Na kama inawezekana kwa nini msichukue hatua sasa kujiandaa na hili suala?

Naweka kalamu chini.

+255626292514
 
Mchanga upo mwingi, sio lazima utoke kwenye mito na unapoita makorongo. Kuna vilima vya mchanga na mawe. Labda useme haja ya kuwa na mitambo ya kushusha milima ya mawe ili kuchonga tofari za mawe zikajenge nyumba.
 
Inawezekana na jibu la kwanza linaanzia kwenye utambuzi wa kemia ya mchanga. Mchanga kikemia ni nini? Mchakato wa kuutengeneza kiasili au kiunde uko vipi?

Swali la pili ni tathmini ya gharama. Ukilinganisha 'mchanga asilia' na ‘mchanga unde’ kipi kinachalipa? Hakuna jambo lisilowezekana, binafsi nakubali; lakini ipo gharama katika kila linalowezekana. Ujenzi unapaswa kuwa nafuu kwa namna yoyote bila kuathiri uthamani ya kusudi la ujenzi husika.

Mchanga upo wa mtoni na upo wa kuchimbwa lakini tabia zake hutokana na mwamba asili ulikuwaje.
Kile kinachoitwa mchanga kwa asilimia kubwa sehemu kubwa kina msimbo wa silika (SiO 2). Kemia ya mchanga inaathiriwa zaidi na mwamba mama. Kwa hiyo, mchanga ni matokeo ya kupondekapondeka kwa miamba husika, na zile chenga kuitwa mchanga.
Kwa hiyo, mchanga unaweza kutengezwa kwa kuponda ponda miamba husika kwa krasha. Inawezekana, shida ni gharama!
 
JE INAWEZEKANA?

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaoishi maisha ya upweke kwa muda mrefu hivyo starehe yangu kubwa baada ya shughuli zangu za kila siku ama ninapopata nafasi ya kumpumzika ni kusoma vitabu.

Hata kabla ya kuandika ninachotaka kuandika siku ya leo mapajani mwangu nilikuwa nimeshika kitabu cha UJASUSI cha muabudu mizimu bwana Yericko Nyerere.

Huko nyuma niliwahi kusoma kitabu kinaitwa ZAWADI YA ADHABU,katika kitabu hicho mwandishi alisema kwamba "hakuna kitu kisichowezekana kufanyika vile tu kufikiria jambo tu inaonesha dhahiri kwamba linaweza kufanyika".

Kwa upande mwingine katika kitabu cha ZERO TO ONE mwandishi anasisitiza kwamba hapa duniani hakuna kitu ambacho binadamu akikihitaji atakikosa ikiwa akakiwekea juhudi.

Kwa kauli mbili za waandishi hapo juu ni dhahiri kwamba sisi kama binadamu tunauwezo wa kufanya jambo lolote ikiwa tutakuwa na nia ya dhati pamoja na juhudi na hizo kauli ndizo zimenipelekea mimi kuandika haya.

Nchi nyingi duniani ikiwepo nchi yetu Tanzania hutumia mchanga katika shughuli zote za ujenzi na mchanga huo hupatikana kwa kuchimbwa ardhini hasa mitoni na makorongoni.

Kila kukicha matumizi ya mchanga yamekuwa yakiongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu majengo yanayojengwa maeneo mbalimbali.

Kwa mtu anayeona mbali ni dhahiri kabisa uchimbaji huu wa mchanga utapelekea uharibifu mkubwa wa mazingira ambao madhara yake yataonekana zaidi katika kizazi kijacho.

Sasa nilikuwa najiuliza je kama nchi tunawezaje kuzuia madhara ya uchimbaji wa mchanga ndipo nikapata wazo la kutengeneza mchanga maalumu kwa ajili ya ujenzi ambao utatengenezwa maabara.

Binafsi mimi sijasoma masuala ya Civil Engineering wala masuala ya chemical processing hivyo nimeshindwa kujibu hilo swala mpaka sasa.

Eti wataalamu wa hayo masuala je inawezekana?

Na kama inawezekana kwa nini msichukue hatua sasa kujiandaa na hili suala?

Naweka kalamu chini.

+255626292514
Huo mchanga upo, kitaalamu tunaita M-sand (yaani Manufactured sand). Huwa unatengenezwa kwa kusaga miamba ya mawe katika ma-crusher kutengeneza punje za mchanga
 
Upunguze kukaa peke yako ona punyeto ilichokufanya
 
Back
Top Bottom