Mchanga wa macho - AY ft. King Crazy GK,Banana Zoro & Complex

Mchanga wa macho - AY ft. King Crazy GK,Banana Zoro & Complex

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
AY FT BANANA ZORO & COMPLEX - MCHANGA WA MACHO ..

CHORUS..( BANANA ZORO)

BANANA ZORO..

"nilijaribu kukupenda na mema mengi kwako nilitenda/


moyoni mwako sikuwapo kumbe ulikuwa mchanga wa macho/

Kwanini uliamua kulisariti langu penzi / sikujua ,ningejua nisingelipoteza wangu muda...


AY ( VERSE..1)


ni bora ungekuwa muwazi ukanieleza wazi wazi/ moyo uka loose nyani matokeo yake yakawa manjozi/ sometime nakaa nawaza mpaka natokwa na machozi/ nikikumbuka mabaya, mazuri tuliofanya Enzi/ umenipa wakati mgumu njia panda sina hamu/ nashukuru umenipa ufahamu wa mapenzi kuwa nao ni sumu/ simu , card na ahadi
Gede gede/ kumbe vyote unazunga ilimradi siku ziende / mwenyewe unafahamu tulivyopendana kabla ujapanda ngazi/ sasa unajiona mjanja kwangu unaleta mapozi/ kuna wakati wazo la kisasi linaniijia uwepesi/ nashinda moyo linaondolewa akilini upesi upesi/ safari njema uendako bado nakuombea mema/ ingawa umenifanyia mambo mabaya kusema/ ulinipeleka mbio sikupata hata muda wa kuhema/ na yote nilifanya kwakuwa kwako nilitwama/ sikupenda ukasirike , wala sikupenda uboleke/ nilipenda ufurahi tukiwa wote wewe ucheke/ kumbe vyote nafanya ni bure ukuridhika/ooh kumbe vyote nafanya ukuwa unavitaka/ ni bora ungeniambia unavyotaka mapema/ au kama ukuridhika mi ningejua la kufanya/ moyo wako umeufunga hutaki niingie tena/ nakubali siwezi force unipende Aina noma mama/...

CHORUS ( BANANA ZORO)

BANANA ZORO..

"nilijaribu kukupenda na mema mengi kwako nilitesa/

" Si ungesema Tu"

moyoni mwako sikuwapo kumbe ulikuwa mchanga wa macho/

"Ungenieleza mama"

Kwanini uliamua kulisariti langu penzi / sikujua ,ningejua nisingelipoteza wangu muda...

Verse 2... ( KING CRAZY GK)

"Like father like a son, like a son na Haki ya mungu nimekubali ya kwamba mapenzi sio mzaa sio mzaa/ na king crazy gk nasema si basi siyataki Tena/ kwani maisha yako matatani/ nimekuwa kama kichaa gk wala silali/ na mbaya zaidi naji kaona kama sifai kuwepo hapa Duniani/ niliyempenda amenikataa kaniacha kwenye mataa/ king crazy nashangaa kisa na mkasa sina fedha/ heyi walimwengu........ni kitu Gani ningelifanya kwake/ ajue ni kweli mi nampenda/ aliyoyafanya kwanza ni mengi lakini haya ya sasa ni mwisho/ mbele ya Wazazi amenikaa sababu ya fedha zimemuandaa/ na kitu cha pili bila kujali penzi lake kwake / mbele ya washigaji akanipa kubwa/ fedha zikamuandaa penzi kwake likawa kama kichaa/ na akanipofua macho wala sikuona hatari Kwa lolote alilolifanya/ na kisha akamuacha mwenye fedha akamwanaa /kama mafungu ya nyanya vesi sokoni kariakoo/ nikipata ninachokitaka ona sasa wamesha mdaka..


CHORUS..
(BANANA ZORO..)


"nilijaribu kukupenda maneno mengi kwako nilitenda/


moyoni mwako sikuwapo kumbe ulikuwa mchanga wa macho/

Kwanini uliamua kulisariti langu penzi / sikujua ,ningejua nisingelipoteza wangu muda...


COMPLEX .. VERSE 3..



Ungenieleza ukweli basi penzi kulitapeli/ unavuta singara sheli unakuja kuniacha feli/ pendo la manati kwako likawa Tamati/ kama chapati ukakunja Kuku ukanipa pati/ Mimi mtanashati kwako nikashuka chati/ matusi na maneno kibao mitaa ya Kati/ mpenzi ungeniambia toka kitambo na Enzi/ nisingefanya ushenzi wa penzi ile kishenzi/ ona sasa balaa muda wote nakosa Raha/ mawazo lukuku kichwani Kwangu hii ni karaha/ tulikuwa sambamba kama maji na samaki/ ona sasa unaniacha pekee yangu mi nahamaki/ hakuna noma hili pingo sasa nakoma/ ulimwengu ndio mama kama jay moe sasa nasoma/ na daka mitungi Kwa wingi nifute mawazo faraja ya muda / muda punde mbele vikwazo/ "hii hatari" napatwa toka mwanzo/ ulipotoa wazo kwamba mi minyenyusho / kupata vizipitisho ulitoa vitisho/ nikifuata nyendo zako sheli utanipa fundisho..


CHORUS..


BANANA ZORO..

"nilijaribu kukupenda maneno mengi kwako nilitenda/


moyoni mwako sikuwapo kumbe ulikuwa mchanga wa macho/

Kwanini uliamua kulisariti langu penzi / sikujua ,ningejua nisingelipoteza wangu muda...

🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶


UKWAJU WA KITAMBO
 

Attachments

  • A.Y._(musician).jpg
    A.Y._(musician).jpg
    593.1 KB · Views: 5
  • images-11.jpg
    images-11.jpg
    24.9 KB · Views: 4
  • images-10.jpg
    images-10.jpg
    18.8 KB · Views: 4
  • images-9.jpg
    images-9.jpg
    54.4 KB · Views: 3
Chorus
Niaminiiii sitochoka kukupenda weee
Mpaka pale nitakaporudi mavumbini
Niamoniii sitochoka kukupenda weee
Licha ya yote yaliyotukutaaa
 
Ipo hiyo nyimbo kwenye album yake ya Mama ya mwaka 2003.
 
Back
Top Bottom