Mchanganuo wa biashara ya bidhaa za urembo kama hereni, kucha, cheni, wanja n.k.

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
747
Reaction score
1,454
Kwa wale members ambao wana uzoefu na hii biashara watupe fununu kuhusu hii biashara maana nina taraji kuianza soon mambo yakiwa mazuri.

Taarifa ambazo ninahitaji kuzifahamu kuhusu hii biashara ni pamoja na 1) Bei ya jumla kwa kila bidhaa hapo mfano bei ya jumla ya hereni za kisasa zisizopauka, cheni, bei ya jumla ya kucha bandia,wanja, lipstick nk

2)Nina hitaji kufahamu namna ya kuweza kugundua ipi feki na ipi ni original, mfano namna ya kugundua hereni zisizopauka, cheni zisizopauka.


3)Nina hitaji kufahamu machimbo ambayo ninaweza nikapata hivyo vitu kwa bei ya chini kabisa, japo katika ule uzi wa wafanyabiashara wanaofanya biashara mkoani wanaochukua vitu kariakoo walitaja location ambayo ni mchikichini lakini ilikuwa juu juu sana hawakutoa information ya kushiba.

Karibuni kwa mawazo na ushauri.
 
Kuna mtaa kariakoo wanauza urembo tu bei rahisi sana, nimesahau jina la mtaa watakuja wataalamu hapa
 
Nenda pale Msimbazi utakuta maduka yote yaliyo upande wa kulia ukiwa unaenda gerezani yanauza vitu vyote unavyovitka tena kwa bei rahisi sana. Hapo ndipo wajanja wote huwa wanachukua urembo n.k
 
Mkuu nenda Mtaa wa mchikichi...jirani na msikiti wa mtoro..unaweza kuhisi uko China...bidhaa zote kutoka China.India..Dubai..utapata hapo...cheni hereni...saa...urembo...chupi...electronics..toys..chupi..vyombo..socks..vipodozi kwa bei rahisi sana.
 
Mkuu nenda Mtaa wa mchikichi...jirani na msikiti wa mtoro..unaweza kuhisi uko China...bidhaa zote kutoka China.India..Dubai..utapata hapo...cheni hereni...saa...urembo...chupi...electronics..toys..chupi..vyombo..socks..vipodozi kwa bei rahisi sana.
chupi za kike zipo
 
bei zikoje?
Bei zinapishana..kila mfanyabiashara ana bei yake kulingana na gharama zake za manunuzi...Ndio maana kabla hujanunua pita kwanza kuulizia bei ya vitu baadaye sasa Ndio unanunua... mfano sox wengine wanauza 8000 kwa dazani wengine 6500, bei pia zinatofautiana kulingana na ubora wa bidhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…