Mungu nisamehe mie. Mchangiaji wa mwisho kwenye maada iliyokuwa inaendeshwa na STAR TV kwa kujitambulisha kwa jina la MJUNI GEORGE NA HUKU SAUTI YAKE NI KAMA ILE YA PIUS MSEKWA hapa nimekoma. Ninamshauri pia atambue hao wanaopiga simu ndo wanamchi wenyewe na haingewezekana wote kupata nafasi ya kupiga simu kwa wakati mmoja. THANKS YAHAYA KWA KUSHTUKIA HILO PIA JAPO BUSARA ZIMEKUTANGULIA NA UKAUCHUNA.
Unapoanzisha mada ni vyema utambue kuwa wana JF wengine hawakusikia hayo majadiliano. Ni vema ukatoa muhtasari wa kilichotokea ndipo ukatoa mawazo yako.
Ni kweli tulikuwa tunasikia mjadala wa star tv kuhusu katiba mpya -mchagiaji wa mwisho aliyejimbulisha kwa jina la mjuni goerge tulitambua kuwa sauti na utambulisho ilikuwa tofauti-pius msekwa tunamfahamu hata kwa sauti -ila alishindwa kujitambulisha wala kubadili sauti yake -lakini hii haitushazi ni yaleyale tunasema moral authority na harakati za kulinda maovu yao.
Hata yahya mhoza alichanganyikiwa kusikia sauti ya mtu anayemfahamu akitambulisha kwa sauti nyingine ambaye alisema wanaochangia mada za katiba watoe maoni yao sio waseme maoni ya wananchi lakini akasahau kuwa yeye ni tabaka lingine na sisi ni tabaka lingine tunaongea tunajua kilio chetu -bahati yake mjadala ulikuwa umekwisha ningepiga na kumwambia saa imefika kuwaweka hadharani na hujuma zao -wamekosa moral authority
Pamoja na kutojua huyo Mjuni alias Msekwa alichangiaje, lakini haina budi ikumbukwe Pius Msekwa ndiye aliyekuwa katibu wa Tume iliyafanya maandalizi ya katiba ya sasa; katika hali hiyo, bila shaka itakuwa vigumu kwake kukaa kimya wakati umma wa watanzania wanaonyesha dalili za wazi za kuihusisha katiba hiyo na kudumaa kwa Tanzania.
...na hasa hasa alikuwa anataka kuwapiga madongo Jeneral Ulimwengu na Mzee Cheyo wa mapesa kutokana na kauli zao kwamba wananchi sasa wako tayari kwa katiba mpya. matokeo yake kwa kutojiamini maana hata yeye alikuwa haamini anachosema akaishia kutaja jina la Uongo sijui akifikiri anamdanganya nani! Hii ndio aina ya Viongozi tulio nao. Anaogopa kutaja jina lake la kweli maana haya yeye mwenyewe ndani ya Moyo wake haamini anachokisema.