Mchango Mh Joseph Mbilinyi(Sugu) toka amekuwa Mbunge kwa vijana wanao tegemea sanaa kama ajira

Ruttashobolwa Zitto ni nani yako mpaka unahangaika hivi kumtetea??? au na wewe ni mmoja wa wale wanaozunguka nae??? haya yote uliyoandika ni baada ya SUGU kumlipua ZITTO..

Kweli Ruta umempatia anampenda Zzk utafikiri anampumulia ikitokea Zzk akaguswa hata kwa upu.mba.vu Wake yeye kuyetea kwa kwenda mbele ilimradi tu kavuta mkwanja kwa zzk msaliti. Rutta wahaya hawafanyi hivyo, ficha up um.bav wako.
 
Wabongo tuna matatizo sana,Zito hawezi kukubali kirahisi tena badala wamsifu wanamponda wakati hili lina manufaa ata kwa wasanii wenyewe ni ngumu sana wasanii kufikia malengo yao
 

Zitto Kabwe ni Mungu mtu maana hakoseagi wala hali rushwa.
 
Mkuu Matumbo achana nao hao wasanii maana washazoea kuchezewa kama ndomu .

Swali ni dogo tu la kujiuliza...Sugu kama msanii kaanzisha umoja wasanii waungane wawe sauti moja wamekataa kujiunga ila Ruge kama promota kaanzisha umoja wa wasanii wote wamejiunga uko...Hivi hapa utamlaumu Sugu au wasanii? ushawahi ona haki ya msanii ikapiganiwa na promota? Yani promota kama sehemu ya tatizo la wasanii ndio anaanzisha umoja wa kupigania haki ya msanii ukiwepo malipo duni na wasanii wanaona uyo ndio mkombozi....hivi awa watu unawasaidiaje jamani? Au walitaka awe anakuja anawapa pesa?....
 

Unajua akili zao za kushikiwa hao mburula.
 

Wewe acha siasa...Sugu kapigana sana kuhusu hatimiliki mpaka ikafikia wakati wakasema hazungumzii jimbo lake bungeni ye kutwa wasanii tu umesahau ilo??..Na kwa taharifa yako ishu ya stika za TRA kwenye kazi za wasanii ili kuzilasimisha at least kama ufahamu ni idea ya Sugu na ndio alioipigania kwenye kamati ya maendeleo vijana na michezo mpaka imepitishwa na serikali sasa utekelezaji hadi leo bado ni danadana..Hivi uyu mtu mlitaka awasaidiaje awa vichwa maji?
 
Kweli nakumbuka hili la stikaa Sugu ndo kalianzisha,wasanii wa bongo wengi hawajielewi.
 

Ndio maana nimehoji kazi ya waziri kivuli ni nini ? hata hao mawaziri kamili huo wana changamoto za majimboni kwao pale wanapowatumikia wanainchi wengine pia kwa nyadhfa zao........so sidhani kama kuna utetezi juu ya hilo.

Angeweza kujenga mshikamano wa wasanii hata wa miokoani, bila kuegemea Dar kama ndio kitovu cha sanaa zote nchini sidhani kama angeweza kuzidiwa nguvu na clouds....na ninamaanisha sanaa zote sio muziki peke yake.

Ni lini wasanii wa mikoani wamewahi japo kumsikia, kutembelewa na yeye mwenyewe au hata kutumia uwakilishi wa wabunge wenzake walipo huko mikoani ?

Sasa kama uwaziri kivuli ni kubeba jina tu na kuandaa budget mbadala hivi kuna umuhimu gani wa kuwa na hao mawaziri vivuli ?

Tunapokosa matumani kwa mawaziri kamili basi walau vilio vya wasanii hao vingesikilizwa na waziri vivuli ?
 
Kweli nakumbuka hili la stikaa Sugu ndo kalianzisha,wasanii wa bongo wengi hawajielewi.
Hili swala la sticker wala haliwasaidii sana wa sanii na ukiangalia kwa sana lina wasaidia serikali kukusanya kodi.

Na ukiangalia wasanii wengi hasa wa bongo flavour hawapeleki Album Sokoni bali wao wanauza single tuu.

Sasa pengine hata Sugu ange hilazimisha serikali na kuishauri kuunda kikosi kazi cha kupambana na wanao burn kazi za wasanii hasa kwenye vibanda kila sehemu nchimi.

Sugu amekuwa yeye ni mtu wa kuchochea migogoro na wadau wa Tasnia hasa muziki na Wasanii wakati alitakiwa afanye kazi ya kuwaunganisha.
 

Mkuu matumbo hatutaki mtu mwenye nia ya kuwagawa watu bali kuwaunganish.

Anacho kosea Sugu ni kutaka kuwagombanisha wasanii na wadau wa sanaa. Tunajua wadau nao wana mapungufu lakini Sugu ana anzisha umoja kwa lengo la kugombanisha watu si kujenga.

Leo hii kwenye mgogoro wa Ruge na Jide ame take side na hili ndio tatizo.

Sugu alitakiwa kuacha mambo ya Malumbano na akajaribu kukaa na Ruge wakajaribu kuwaunganisha wasanii.

Hivi kwanini tuamini kuwa wanao gombana na Ruge hawajamkosea Ruge?

Kwakweli tukiacha migogoro Sugu hana mchango kwenye tasnia ya muziki.
 
Last edited by a moderator:

Je kama Ruge ndio tatizo kwenye hili unataka sugu afanye nini... how sure kuwa Sugu ndiye anaye wagawa and not Ruge.... haya tumeona Ruge na Sugu wakipatanishwa wakati huohuo Jide akikosana na Ruge hapa nani mwenye tatizo na kwanini promota ndio awe msemea wa sanii na sio wasanii wenyewe who is Ruge????
 
Last edited by a moderator:

Ndio maana nawaambia nyie hamna lolote mnafanya siasa za kumchafua Sugu tu hapa.... Yani unataka Sugu apige marufuku uchomaji wa cd kwa mamlaka yepi na serikali kaipigia kelele tangia sio mbunge na mpaka kawa mbunge,sasa kama serikali haitaki yeye afanyeje??.....Ngojea nikupe elimu kuhusu stika za TRA bab,bidhaa kama dvd au cd ukiwa na stika ya tra inakuwa kitu rasmi kinachokatwa kodi....advantage yake kwa wasanii ni kuwa haitakuwa kazi ya msanii kupita mitaani kukamata cd feki,itakuwa ni tra wanakamata bidhaa feki zinazokwepa kodi....Ni kama unavyoona konyagi isiyo na stika ya tra ukikamatwa nayo ni msala,konyagi hawapiti mtaani kukamata konyagi feki bali tra ndio wanafanya hivyo....hapa cd feki au bidhaa yoyote feki ya sanaa itashugulikiwa na tra
 

Vilio vya wasanii wa mikoani ni vipi ambavyo viko tofauti na hawa wa dar hata afande Sele pia ni wamkoani maana maisha yake yote yako Moro na Mike t pia na Soggy Doggy pia hawa ni wasanii wa mikoani...

Suala ni je kunajipya gani Sugu hajalisemea kuhusu wasanii... je hiyo serikali yenu sikivu imewafanyia nini tangu Sugu asome hotuba ya waziri kivuli since 2011 to 2014 yapi wameyatimiza kwenye hotuba zake japo kaongea sana.

Issue ya studio mkaona bora mumpe promota Ruge wakati harakati alizianza Sugu na wasanii wasiojielewa baada kumuunga msanii mwenzao ili wamiliki studio wakamuunga yule promota ili studio aihamishie kwenye nyumba yake ya vipaji.


What do you need from Sugu wakati hao wasanii mnaosema hawasaidii wenyewe hawataki hata kumsikia akili na masikio yao yapo mawingu kwa promota wao.
 

Hivi we una akili kweli?? Akae na Ruge awaunganishe wasanii kwani Ruge ni nani ivi ujioni ulivyo mjinga.....toka lini promota akawa mtetezi wa wasanii??promota ndio awaunganishe wasanii? hivi ujui kuwa mapromota ndio sehemu ya tatizo la wasanii....wasanii wangapi wanamlalamikia uyo ruge alafu unasema eti wakae pamoja ili wafanyaje sasa? ...mtu anajaribu kurekebisha mfumo au ulitaka awagawie hela au? nani kakwambia tatizo la wasanii ni ugomvi kati yao?...tatizo la wasanii ni kipato ,watakuwaje na uhakika wa kipato ni kuubadili mfumo huu mbovu...
 
Last edited by a moderator:

Sugu anaweza akawa haungwi mkono kwa sababu ya mwenendo wake wakupenda migogoro na wadau na hata wasanii.

Anatakiwa aache kukaa kwenye migogoro na awe kiungo na kuhakiKisha watu wana fanya kazi kwa Amani.

Ukiangalia kwenye Mgogoro wa Ruge na Jide, Sugu alichukua upande ambapo tulitegemea angekuwa wa kwanza kuhakikisha Amani kati yao ina patikan.

Yani wanataka kutuaminisha kuwa Jide hana tatizo bali ni Ruge.
Natunajua Ugomvi wa Ruge,Jide na Sugu una rudisha tasnia nyuma maana hawa wote ni watu muhimu na wana wafuasi wengi nyuma yao.

Ruge anaonekana wazi kutaka Amani na hawa watu lakini wao hawataki na Sugu ana nafasi ya kutafuta suluhu lakini yeye amekuwa akifurahia watu wakisema usinizike,sijui kwenye msiba wangu usije.



Kwakweli Sugu ana penda sana Migogoro.
 

Kwanza Ruge ni nani mpaka wakae nae tz ina vyombo vya habari zaidi ya 100... who is Ruge by the way mpk wapatane.. Ruge akizingua radio nyingine zipo... nashangaa jamaa analeta hoja kisa tu Sugu hana mahusiano mazuri na Ruge. Angekuwa hapatani na wakurugenzi wa radio nyingine wote sawa ila Ruge tu basi yeye ndo anamatatizo, iweje agombane na kila msanii
 
Mkuu huu mjadala ukitaka uende vyema achana na lugha hizo na zinaonesha unaanza kupoteza uelekeo.Mimi hata sikumoja sijadili kwa kutumia lugha hizo

Back to topic




Nimemsema Ruge sababu hatuwezi kujidanganya kuwa si mdau wa sanaa hii na hata kungekuwa na Mgogoro na Mengi ninge sema akae nao mambo yatafutiwe suluhu maana wao wana miliki vyombo vya habari na ndio wadau na bila wao hizo nyimbo tunge zisikia?

Hakuna njia nyingine mpaka tuoneshe kuwa hao watu ni wabaya mpaka kutengemeza makundi ya kuwa tukana?

Hivi kweli hao unao waita mapromota hawna uzuri wao?
Ni wabaya tuu?
 

Ndio maana amepewa hiyo wizara anatakiwa kutoa ushauri kwenye hilo jambo.

Pia anaweza kuongea na waziri mhusika, tatizo ni kuchukulia upinzani ni uugomvi.

Kama kweli Sugu ange amua kuweka chuki na migogoro yake pembeni wasanii wange nufaika sana na uwepo wake pale bungeni.

Hata kutoa ushauri kwa serikali kuunda kikosi kazi inge saidia sana sio kuzua migogoro tuu.
 

Mzee wa visasi, wivu, ubaguzi, kujisikia, fitina. Hahahaaa ...!!!πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…