Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Heshima kwenu!!
Aina binadamu ziishizo katika ulimwengu huu wa Leo ni matokeo ya ubora na udhaifu wa aina binadamu katika zama zilizopita.
Kuna aina nyingi za namna mbalimbali za binadamu. Kutokana na uwepo wa aina hizi ambazo zina utofauti wa maumbile, lugha, rangi, Vimo, tabia na mienendo Leo hii wale waonekanao ni bora kwa sifa zao hukandamiza Uhuru wa binadamu wengine wenye sifa zichukuliwazo kuwa ni dhaifu.
Katika kufikiri kwangu, nilipata kujua mambo kadha wa kadha ambayo yamemfanya mwanadamu aliyekiumbe huru kujiingiza katika utumwa usio kifani.
Aidha mwanadamu alipaswa awe kiumbe kamili mwenye mamlaka kamili ambaye hujitawala pasi na msaada wowote kutoka nje.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyomfanya mwanadamu aliyekiumbe huru kuingia katika gereza la utumwa;-
1. Imani.
Imani ni jawabu la mambo ya kufikirika, ambayo hutuliza hofu, na woga kwa huyo mwenye nayo. Imani ni matokeo ya woga wa jambo ambalo hutarajiwa kutokea hivyo imani hutumika kama njia ya kufariji na kutoa matumaini kwa siku zijazo.
Chanzo cha imani.
-Woga wa mambo yajayo ambayo hayathibitiki
Ili mtu Fulani awe na imani ni lazima awe na woga wa mambo ambayo hayathibitiki. Mambo hayo husimuliwa na watu fulani kwa malengo fulani, mambo hayo husimuliwa kwa lugha tamu zenye utisho. Pia ili aweze kuamini basi sharti la kwanza ni kumgopesha ili woga umfanye asiwe na matumaini. Hatua inayofuata baada ya mtu kuwa mwoga na kukosa matumaini katika hatima yake, mtu huyo hupewa ahadi za matumaini zenye faraja na hapo ndipo Imani huzaliwa.
Hata ukienda kwa waganga wa kienyeji hutumia njia hii hii ya kukutia woga ili ukose matumaini, hufanya mauzauza na kuongea lugha za kutisha ili uogope kisha hukwambia kuwa anaweza kukusaidia.
Hadithi za mababu zetu zilijengwa kwa misingi hii ili kuleta woga ambao humfanya mtu asiwe guru
2. Imani kuikandamiza Akili.
Imani hudumaza uwezo wa kufikiri. Na mtu ajihusishaye na imani si rahisi kuwa huru. penye Imani kuna miiko na Sheria. Wakat penye akili hakuna miiko, na sheria hufikiriwa kulingana na Muda na Mazingira.
MTU afikirishaye akili yake huwa huru zaidi ya MTU mwenye Imani.
Jamii moja huweza kuikandamiza jamii nyingine kwa kuathiri Imani ya jamii Fulani kisha kudumaza uwezo wa kufikiri.
Wakoloni walipofika eneo lolote duniani kitu cha Kwanza kukidumaza kilikuwa ni Imani ya watu wa sehemu husika. Imani huamua maisha ya watu, vile walavyo, wanywavyo, wavaavyo n.k Imani huzaaa utamaduni, kisha mila na desturi.
Wazungu walikusudia kuleta imani mpya ambayo ingeathiri Akili ya mtu mweusi(Muafrika). Mtu akishakutawala kile unachoamini ametawala Akili yako. Hapo ndipo walipoleta Elimu ya kizungu isiyo na manufaa kwa watu weusi.
Kama wazungu wasingekuja Afrika basi Afrika ingekuwa mbali sana kimaendeleo.
Kwa kifupi ni kuwa, Mwafikra ili awe huru na ajiondoe utumwani basi Sharti ajitoe kwwnye masuala ya imani. Atumie akili kukabiliana na Mazingira.
Watu wanaotumia imani ni kama hayawani wa kufugwa na mwituni.
Hata mfano Alioutoa Yesu kuhusu ndege yakuwa hawavuni wala hawapandi lakini Mungu huwapa Chakula. Mfano huu ni kwa Ulimwengu wa kale ambao watu hawakufikiri jambo jingine zaidi ya Chakula, malazi na mavazi.
Lakini Ulimwengu huu huwezi kutumia Imani kubuni ndege, au Teknolojia yeyote. Imani hutumika kwa vitu ambavyo ni vya asili na Msingi wa Maendeleo ni Man-made features kama Barabara, Mabenki, shule, na huduma zingine za kijamii.
Mataifa yalioendelea yalipitia hatua za kupinga au kuweka mipaka kati ya mambo ya kiimani na mambo halisi. Mengine yalifuta kabisa na kutotambua uwepo Wa Mungu.
Ikumbukwe kwamba Mungu ananafasi ndogo katika Maamuzi ya watu katika jamii. Na Maamuzi humtofautisha mtu mmoja na mwingine katika maendeleo ya Maisha.
Kwenye Imani hakuna Utafiti.
Baraka ni Kanuni halikadhalika Laana.
Hivyo Afrika haiendelei kwani watu wake huweka imani mbele bila kujua kuwa inamchango mdogo kwenye maendeleo.