Moto mingi
Member
- Jun 13, 2023
- 7
- 6
1.Historia ya ukuaji wa teknolojia
Teknolojia ni utumiaji wa maarifa ya sayansi kwa ajili ya kubuni, kuunda, kuboresha na kutumia zana, vifaa, mifumo, na michakato ya kufanyia kazi ili kuchangia maendeleo katika maisha ya binadamu au katika utendaji wa shughuli zozote za kibinadamu kwa uharaka na ufanisi mkubwa. Teknolojia inatumiwa katika sekta zote ikiwemo viwanda, usafiri, mawasiliano, afya, elimu, kilimo, na nishati na kadhalika
Katika karne ya 4 KK (kabla ya Kristo) mwanasaikolojia Aristotle alitunga
neno la Kigiriki la "technologia" na akagawanya maarifa ya kisayansi katika sehemu tatu: sayansi ya nadharia, sayansi ya vitendo, na sayansi ya uzalishaji (teknolojia).
Teknolojia imekuwa ikikua kwa kasi sana duniani kote katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Ukuaji huu unahusishwa na maendeleo ya kasi ya sayansi, utafiti wa hali ya juu, na uvumbuzi wa teknolojia mpya. Leo, teknolojia ni nguvu kubwa inayo gusa maisha ya watu katika sehemu zote za dunia.
Nchini Tanzania, teknolojia pia imekua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Serikali ya Tanzania imejitahidi kuhamasisha maendeleo ya teknolojia na uvumbuzi kwa kuwekeza katika miundombinu ya teknolojia, ikiwa ni pamoja na miundombinu mbalimbali kama vile miundombinu ya umeme wa uhakika, na nishati mbalimbali kama vile mafuta ghafi mfano mwezi wa tatu 2023 shirika la itangazaji la BBC
walichapisha habari. (13 Machi 2023)
"Tanzania na Uganda zimeanza kutekeleza ujenzi wa bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,400 unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2025". Mradi huo utagharimu zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 na unatarajiwa kuzalisha zaidi ya mapipa bilioni moja kwa kipindi cha miaka 25 ijayo. Pia kuna uwekezaji katika elimu (katika sekta ya teknolojia) katika
kuhamasisha uvumbuzi wa ndani.
2. Changamoto zinazo ikumba nchi yetu ya Tanzania Katika kukuza teknolojia
Serikali ya Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa katika kukuza teknolojia, ikiwemo upatikanaji wa rasilimali za kutosha za kifedha, vipaji na ujuzi wa kutosha katika taaluma za teknolojia, na miundombinu ya teknolojia ambayo haijaendelezwa.
Serikali inapaswa kuwekeza zaidi katika uelewa na mtazamo wa muda mrefu wa teknolojia ili kusaidia kuendeleza teknolojia na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi."
3.Jitihada za serikali katika kukuza teknolojia nchini
Katika kuimarisha Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Maendeleo ya Taifa Serikali imeendelea kuchochea maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa kuwatambua na
kuwaendeleza wabunifu nchini kwa lengo la kuchangia maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
Katika kufikia azma hiyo, Serikali imetekeleza yafuatayo: Imetoa mafunzo kwa wabunifu wachanga 83 na rasilimali fedha kwa wabunifu 27 walioibuliwa katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu(MAKISATU) mwaka 2022 kwa lengo la kuendeleza bunifu na teknolojia ili zifikie hatua ya ubiasharishaji; na Imetambua teknolojia mpya 27 zilizozalishwa nchini na hivyo kufanya jumla ya teknolojia zilizotambuliwa nchini hadi sasa kufikia 506. Lengo la utambuzi huo ni kuwa na kanzidata ya kitaifa kwa ajili ya rejea kuhusu taarifa za teknolojia na ubunifu zinazozalishwa nchini (Waziri wa elimu sayansi na teknolojia profesa Adolf Mkenda may 2023 ).
Hii inaonyesha jinsi serikali inavyo jitahidi kukuza na kuendeleza teknolojia nchini.
4. Mchango wa kujenga teknolojia shindani nchini Tanzania
Kujenga teknolojia shindani nchini Tanzania kuna mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na ustawi wa nchi.
Kwa kuwa teknolojia shindani ni ubunifu wa kuboresha bidhaa, huduma, na mchakato wa kuzalisha na kutoa bidhaa na huduma kwa haraka, zenye ubora wa kiwango cha juu na gharama nafuu kwa watumiaji. Teknolojia shindani inasaidia kuongeza tija, kupunguza gharama za uzalishaji na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Sekta kama kilimo cha jembe la mkono kiurahisi kabisa sekta hizo zitachukiliwa na mashine ambazo zitarahisisha Kazi na kupunguza muda hivo kumfanya mkulima kumfanya majukumu mengi ndani ya muda mafupi Sana hivyo kukuza kipato na uchumi kiujumla
Akielezea umuhimu wa kujenga teknolojia shindani, Mtaalam wa TEHAMA na Meneja wa Mradi wa Sayansi na Teknolojia wa Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo (IITA) Dokta(DK)Christopher Materu alisema: "Tanzania inahitaji kujenga teknolojia shindani ili kushindana na nchi nyingine ulimwenguni kwa sababu teknolojia inayojengwa na kuzalishwa ndani ya nchi itaendelea kuhimili kwa muda mrefu, hivyo kuokoa fedha za kununua teknolojia kutoka nje na itasaidia kuongeza mapato ya ndani kwa kuuza teknolojia nje ya nchi."
Kwa hiyo, kujenga teknolojia shindani nchini Tanzania kutawezesha nchi kushindana kwa ufanisi katika soko la kimataifa na kuchangia katika kuimarisha uchumi wa nchi.
5. Serikali iongeze nini zaidi ili kufikia teknolojia shindani zaidi?
Kutoa ufadhili na ruzuku kwa wajasiriamali wa teknolojia wa ndani kuwezesha kukuza na kuboresha bidhaa zao. Serikali inaweza kutoa mikopo nafuu na ruzuku kwa ajili ya utafiti, maendeleo na ubunifu kupitia taasisi za serikali na vibali vya biashara
Kuanzisha sera na mikakati ya kuwahakikishia wawekezaji kuwa wana uhakika wa usalama wa uvumbuzi wao na biashara zao. Serikali inaweza kuanzisha sheria zinazolinda hakimiliki na hakishiriki katika uvumbuzi ili kuvutia wawekezaji katika sekta ya teknolojia.
Kupunguza tozo na ada kwa wajasiriamali wa teknolojia. Serikali inaweza kupunguza kodi na ada kwenye huduma za mtandao ili kufanya biashara za teknolojia kuwa sahihi kifedha.
Kuendeleza na kukuza wataalam wa teknolojia. Serikali inaweza kuendeleza taasisi za utafiti wa teknolojia na kuanzisha kozi za teknolojia katika vyuo kusaidia kuendeleza wataalam wengi katika uwanja wa teknolojia.
Kwa kufanya yote haya, serikali ya Tanzania itakuwa imejenga mazingira wezeshi ambayo yatakuwa na athari chanya kwa wawekezaji na wajasiriamali wa ndani, kusaidia kufikia teknolojia shindani zaidi duniani.

Upvote
5