Mchango wa mawazo juu ya kurudisha mkopo

Joined
Jun 29, 2015
Posts
15
Reaction score
9
Habari wanajamvi,
Kuna mfanyakazi mwenzangu hapa ofisini alikopa kam mill.4 kwenye hizi financial institutions alitakiwa arudishe 5.6m pamoja na riba kwa muda wa miezi kumi kila mwezi ni sh.560,000 ameshalipa miezi minne mil.2,240,000, bado mil.3,360,000, hivi juzi jamaa kapata milioni 6 kutokana na mgao wa mauzo ya shamba lao la urithi, je anaomba ushauri alipe deni lote kwa wakati mmoja au aendelee kulipa kwa kila mwezi ili hizo hela afanye investment, aliongea na credit officer akasema hakuna excemption yoyote ile kwa kuwahi kulipa mkopo.

Mimi nimemshauri afanye investment kwani mkataba wa mkopo ulikuwa unategemea mshahara, nakaribisha mawazo yenu manajamvi.
 
Afanye mambo mengine na hiyo pesa ila awe na uhakika wa kusimamia hiyo kazi...la, alipe deni aendelee kutegemea mshahara! All in all...afanyie something productive!
 
umemshauri vizuri, asilipe mkopo kwa mara moja aendelee kulipa kidogo kidogo
 
kulipa kwa mkupuo mkopo hupunguza kiwa cha riba, kwasababu amelipa kabla ya muda uliopo kwenye mkataba, so anaweza akalipa ili apunguziwe hiyo riba... kinachobaki afanye investment... pesa ambayo inakuja vuuuup then hujaipangia cha kufanya, utakula bata weeeee na shoping za hatareeeeeee then inakula kwako...
 
Mie pia namshauri ainvest,maana kama inategemea mshahara basi haina shida.
Ingekuwa amejiajiri kama mie,basi leo leo ningelipa,maana maisha ya kujiajiri kwenye mikopo ni majanga.

Ila kama yupo kwenye ajira,mwambie akilipa deni lote atakuwa amefanya kosa kubwa saana katika maisha yake unless awe hana Idea ya biashara kichwani.


A Invest pesa hiyo,na atagundua kwamba hiyo 3.4m iliyobakia inajilipa yenyewe kwenye deni bila kujua.
Sasa atakuwa na advantage kwamba hiyo 3.6 ameyotaka kuilipa kwa mkupuo ndio hiyo itajilipa deni loote kama aki invest na pia atakuwa amebakia na mtaji wake pale pale.
 
Pengine ni vzr akalipa deni/mkopo kwa mkupuo ili aweze kukwepa riba. Hiyo taasisi kama inasema akilipa kwa mkupuo hakuna unafuu basi ni kampuni ya "kitapeli". Pesa atakayobakiza ndio aende akaanzishie biashara. Biashara hasa hizi ndogo ndogo hua sio vzr kuzianza kwa pesa ya mkopo. Biashara ina sura nyingi hivyo ni vzr ukaianza kwa pesa yako then ikisimama basi unatafuta mkopo kwa kuzingatia mahitaji ya biashara husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…