Mchango wa Mbunge Ameir Abdallah Ameir kuhusu wataalam wa hali ya hewa

Mchango wa Mbunge Ameir Abdallah Ameir kuhusu wataalam wa hali ya hewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. AMEIR ABDALLAH AMEIR, Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Akizungumza katika Kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni jijini Dodoma kwa Wizara ya Uchukuzi na kujibiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile.

"Serikali huwatambua Wataalam wa Hali ya Hewa na kuwapa madaraja kwa kuzingatia vigezo viwili; Elimu (Academic Qualifications) na Uwezo (Competence) kwa kutekeleza majukumu mbalimbali ya Hali ya Hewa.

"Kwa mujibu wa muundo wa Kada ya Hali ya Hewa, Serikali inawatambua Wataalam wa Hali ya Hewa katika madaraja matatu; Mtaalamu Msaidizi wa Hali ya Hewa (Elimu ni AStashahada[Certificate], Stashahada [Diploma] ya Hali ya Hewa au fani nyingine inayohusiana na Hali ya Hewa kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali; Mtaalamu wa Hali ya Hewa anayekuwa na ngazi ya Shahada (Degree); na Mtaalamu mbobezi wa Hali ya Hewa mwenye ngazi ya Shahada ya Uzamili" - Mhe. David Mwakiposa Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi

"Kwa kuwa Serikali inatumia gharama kubwa sana kuwasomesha Wataalam wa Hali ya Hewa, hivi sasa wamekuwa ni msaada mkubwa katika kutunusuru na majanga na mabadiliko mbalimbali ndani ya nchi na wengine wamehama kutokana na maslahi madogo, Je, Serikali haioni kwamba imefika wakati kuwaona kwa jicho la huruma ili wafanye kazi kwa ufanisi zaidi?" - Mhe. Ameir Abdallah Ameir

"Kumekuwa na kukaimu kwa Mkurugenzi kwa kipindi kirefu katika Mamlaka ya Hali ya Hewa jambo ambalo linazorotesha utendaji, Je, ni kipi ambacho kinasababisha hali hii?" - Mhe. Ameir Abdallah Ameir

"Tunaboresha Incentive Package za taasisi sambamba na kuongeza maslahi yao hatua kwa hatua, mwaka kwa mwaka kwasababu mahitaji ya nchi yetu ni makubwa. Tunaongeza kidogo kidogo kutokana na Rasilimali fedha" - Mhe. David Mwakiposa Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-04-17 at 20.03.39.mp4
    19 MB
  • WhatsApp Image 2024-04-17 at 19.59.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-17 at 19.59.40.jpeg
    58.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom