Mchango wa Mr. Blue ni mdogo sana, watu wafuatao kwa maoni yangu hawapaswi kusahauliwa kwenye historia ya Bongo fleva. 1. Saleh Jabri, Balozi, Sugu, kwanza unit n.k hili ni kundi LA waanzilishi (late 1980's up to 1990's) 2. Inspector Haroun na Prof J (late 1990's -early 2000's) hawa wawili walitoa mchango mkubwa katika kubadilisha mtazamo wa watu dhidi ya bongo fleva, wimbo wa Inspector mtoto wa geti Kali uliwafanya mabraza men na wanawake wengi waanze kuupenda mziki wa kizazi kipya, nikumbushe tu hakuna wimbo wa bongo flavour uliokaa kwenye chati kwa muda mrefu katika radio mbali mbali kama huu. Prof. J akijulikana kama Nigger J enzi hizo na kundi lake hard blasters na wimbo wao Mola nitoe roho ulileta mapinduzi katika ujumbe wa mziki. 3. MB doggy(Mid 2000's) Huyu alileta msisimo mkubwa na nyimbo yake ya Latifa, naweza kusema huyu ndie baba wa "wabana pua". Baada ya mafanikio makubwa ya Mb doggy taratibu mziki wa kufoka foka ukaanza kumezwa na wale wa kuimba, waimbaji wengi kama matonya, voice wonder n.k wakaibuka. kwa mtazamo wangu hao ndio watu wenye mchango mkubwa katika transformation ya bongo flavour.
n.b mods mnaweza kuanzishia Uzi mchango huu kama mtaona yafaa.