UTANGULIZI
Siasa ni sera ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji,taifa au hata kujumuisha dunia kwa ujumla. Kuna sababu kazaa za kulazimisha kwa nini ushiriki wa wanawake Katika siasa ni mhimu na una matrokeo chanya kwa demokrasia kuanzia katiaka ngazi ya familia,jamii , taifa na duniani kote kwa ujumlaUshiriki katika siasa kwa upande wa wanawake unashuhudiwa kuongezeka kadri ya mda unavyoenda.
Kulingana na taarifa kutoka “muungano baina ya mabunge”duniani “INTER-PERLIAMENTARY UNION” (IPU) ,inayoonesha ya kuwa wanawake kote duniani wanachukua asilimia 26.9% ya viti katika bunge zote duniani ya 2024 januari. Hii inaonyesha ya kuwa kuna ongezeko la ushiriki wa wanawake kadri ya mda unavyoenda ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Mchango wa wanawake katika siasa umekuwa na umuhimu mkubwa katika kuleta mabadiliko na kukuza demokrasia katika jamii mbalimbali duniani kote.
View attachment 3022666
View attachment 3022667
Chanzo; Inter-Parliamentary Union ,ukr.14-15
MCHANGO WA WANAWAKE KATIKA SIASA
1. Uwakilishi na Ushiriki katika Serikali na Bunge;
Ushiriki wa wanawake umesaidia kuboresha uwakilishi wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi. Wanawake wanapoingia kwenye nafasi za uongozi, wanaweza kuwakilisha maslahi ya wanawake na watoto, na kuleta mtazamo tofauti kuhusu masuala ya kijamii na kiuchumi. Wanawake wamepiga hatua kubwa katika kuongeza uwakilishi wao katika nafasi za kisiasa. Kwa mfano, katika nchi nyingi, idadi ya wanawake wanaohudumu kama wabunge au mawaziri imeongezeka katika miongo ya hivi karibuni. Hii imekuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha sauti za wanawake zinasikika na maslahi yao yanawakilishwa ipasavyo.
2. Kuleta ajenda za Kijamii na Maendeleo;
Wanawake mara nyingi wamekuwa mstari wa mbele katika kuibua masuala ya kijamii na maendeleo katika siasa. Wamekuwa mabalozi wa masuala kama elimu, afya, haki za wanawake, na usawa wa kijinsia. Kupitia ushiriki wao katika siasa, wanawake wameweza kuleta mabadiliko chanya katika sera za umma zinazogusa maisha ya wananchi wengi.
3. Kupigania Haki za Wanawake
Wanawake wamekuwa wakipigania kupitishwa kwa sheria na sera zinazolinda na kuboresha haki za wanawake, ikiwa ni pamoja na haki za kiraia, haki za kisiasa, na haki za kiuchumi. Mifano kama vile harakati za wanawake za kupigania haki ya kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi ni ushahidi wa jitihada zao katika kuboresha demokrasia.wanawake wamekuja kauli mbiu yao ya “HAKI SAWA KWA WOTE” ambayo inahimiza usawa wa jinsia katika jamii
Chanzo;mahakama ya Tanzania 2017 march 9
4. Uongozi wa Kiafya na Usimamizi
Wanawake wameonyesha uongozi mzuri katika kuongoza na kusimamia masuala ya afya mfano mizozo ya kiafya. Ushiriki wao katika ngazi za juu za serikali na mashirika ya kimataifa umesaidia kuleta ufumbuzi wa kibinadamu na maendeleo endelevu. Mfano uongozi wa DK. UMMYY ALLY MWALIMU katika kusimamia janga la COVID-19 inaonyesha umuhimu wa uongozi wa mwanamke katika nyakati za mgogoro.
5. Sera za Kijamii:
Wanawake mara nyingi wamekuwa mstari wa mbele katika kusukuma sera za kijamii zinazolenga maslahi ya familia, afya, elimu, na ustawi wa jamii kwa ujumla. Mchango wao umesababisha maboresho katika sera za elimu, afya ya uzazi, na ulinzi dhidi ya ukatili wa kijinsia.
6. Usimamizi na Uwajibikaji:
Ushiriki wa wanawake umesaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mifumo ya kisiasa. Wanawake mara nyingi huwa na uwezo wa kuunganisha pande mbalimbali na kusuluhisha mizozo kwa njia ya majadiliano na utaratibu.mfano raisi wa jamhuri ya Tanzania MH. SAMIA SULUHU HASANI kwa usimamizi na uwajibikaji wake juu ya maendeleo katika nyanja mbalimbali yaani kiuchumi ,kisiasa,kijamii na hata kidini.
7. Kuimarisha Demokrasia:
Ushiriki wa wanawake katika siasa umesaidia kuimarisha demokrasia kwa kuongeza idadi ya watu wanaoshiriki katika mchakato wa maamuzi ya kisiasa na kuongeza uwakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii.
CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WANAWAKE KATIKA SIASA
1. Kutokuwepo kwa Msaada wa Kutosha
Katika baadhi ya maeneo, wanawake wanaweza kukosa msaada wa kifedha, mafunzo na rasilimali nyingine muhimu ambazo zinahitajika ili kuongeza uwakilishi wao katika siasa. Wanawake mara nyingi wanakabiliwa na uhaba wa rasilimali za kifedha, msaada wa kisiasa, na fursa za kujitokeza katika nafasi za uongozi.
2. Mfumo Dume
Mfumo dume unaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya wanawake katika siasa. Tamaduni na miundo ya kijamii ambayo inathibitisha madaraka ya kiume inaweza kuzuia upatikanaji sawa na usawa kwa wanawake katika siasa.
3.
Ubaguzi na Itikadi za Kijinsia:
Wanawake mara nyingi hukabiliana na ubaguzi na itikadi kali za kijinsia ambazo huwazuia kushiriki kikamilifu katika siasa.
4. Uwakilishi na Mipango ya Kijinsia:
Mifumo ya kisiasa mara nyingi haina uwakilishi mzuri wa wanawake, na mipango ya kijinsia inaweza kuwa dhaifu au isiyo na nguvu.
5. Utamaduni na Taratibu za Jamii:
Tamaduni na taratibu za kijamii mara nyingi huweka vikwazo vya kitamaduni ambavyo vinaweza kuwazuia wanawake kushiriki kikamilifu au kuchukuliwa kwa umakini katika siasa.
6. Ubaguzi wa Vyombo vya Habari:
Wanawake wanaweza kukosa uwakilishi mzuri au kuchukuliwa kwa njia isiyo sawa na vyombo vya habari, ambavyo ni muhimu kwa kujenga umaarufu na uungwaji mkono katika jamii.
HITIMISHO
Wanawake katika siasa ni chachu ya maendeleo.hivyo basi wanawake tunatakiwa kuwaamini ,kuongeza uwakilishi wa wanawake juu ya mahitaji ya raia,kuhamasisha ushirikiano baina ya pande za vyama vya siasa juu ya ushiriki wa wanawake. Uongozi wa wanawake unaweza kujenga siasa na demokrasia iliyo imara katika jamii ,taifa na duniani kwa ujumla. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa KOFI ANNAN aliwahi kusema”utafiti baada ya masomo umetufundisha ya kuwa ,hakuna zana ya maendeleo yenye ufanisi zaidi kuliko uwezeshaji wa mwanamke”
Hivyo basi ni mhimu kwa jamii kuendelea kuunga mkono na kuhakikisha kuwa sauti za wanawake zinasikika na maoni yao yanazingatiwa katika maamuzi ya kisiasa. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuleta mabadiliko endelevu katika jamii zetu na kuimarisha demokrasia kwa ujumla na ndiyo maana wanawake wanakauli yao ya “TUKIWEZESHWA TUNAWEZA” kwa hiyo ni mhimu kuongeza ushiriki wa wanawake katiaka siasa, kikubwa ni kuwaheshimu na kuwathamini lakini sio kuwadharau.
Upvote
4