SoC01 Mchango wa Sekta ya Elimu katika maendeleo

SoC01 Mchango wa Sekta ya Elimu katika maendeleo

Stories of Change - 2021 Competition

MTEGULE

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
15
Reaction score
22
Sekta ya elimu ni mojawapo ya sekta nyeti sana katika maendeleo ya kila taifa hapa ulimwenguni ikiwemo Taifa la Tanzania. Hili lipo wazi na hakuna wa kupinga kwani zipo ithibati nyingi dhahiri zinazobainisha suala hilo.

Katika nyanja zote za uzalishaji mali kama vile ufugaji, kilimo,biashara, uvuvi, usafirishaji, uchimbaji wa madini,utalii, uamarishaji wa viwanda na nyingine nyingi ambazo humsaidia mwanadamu kukidhi mahitaji yake na kuishi maisha bora.Shughuli zote hizo za uzalishaji mali ili ziweze kuendelea na kukua vema zinahitaji wataalamu wazuri na wabobezi ambao ndiyo watatoa mwongozo sahihi kwa jamii ni kwa namna gani uzalishaji ufanyike ambao utakua ni wenye tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa zima kwa ujumla.

Elimu ni maarifa au ujuzi ambao huweza kutumika katika jambo fulani ambalo huendana na kazi hiyo, katu huwezi kutenganisha elimu na shughuli nyingine za uzalishaji mali pamoja na masuala muhimu ya maendeleo ya jamii.Tunaweza kusema kwamba Elimu ni kama baba katika familia kwani ndiye hutoa mwongozo na maamuzi ili kuweza kufikia lengo.

Katika Sekta hii ya elimu ningependa kuzungumzia kwa mawanda mapana kabisa hasa watu au wafanyakazi wanaohusika moja kwa moja na utoaji wa elimu au ujuzi na maarifa kwa wanajamii hasa wanafunzi kutokea ngazi ya shule ya msingi, ngazi ya sekondari hadi ngazi ya juu ya chuo kikuu ambao ni Walimu.

Walimu ni wafanyakazi ambao wana mchango mkubwa mno katika jamii yetu ya Tanzania na dunia nzima kiujumla katika kuzalisha wataalamu na wasomi mbalimbali ambao hufanya kazi katika mashirika,taasisi na makampuni mbalimbali ya umma na binafsi na kuwapatia wanajamii huduma iliyokuwa bora na kwa kiwango cha juu.

Hatuwezi kupata madaktari bingwa, wahandisi wa shughuli mbalimbali, wahasibu wazuri, mabaharia na warusha ndege angani, wataalamu wa kilimo na mifugo, wataalamu wa tafiti mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya jamii isipokuwa lazima wapitie kwa Mwalimu ambaye huwa na kazi kubwa mno ya kutoa na kupandikiza maarifa na ujuzi kwa wataalamu hao.

Kikubwa cha kushangaza na kustaajabisha zaidi, jamii yetu hasa jamii ya kitanzania imemuweka mwalimu na kumchora mwalimu kama ni mtu duni, aliye na thamani ndogo na pengine hana Umuhimu.Wahenga waliwahi kunena kwa kusema "Huwezi kuijua na kuitambua Neema ikiwa upo nayo" hili linadhihirika wazi kwa jamii ya kitanzania.

Hapana shaka ni kasumba na ni fikra ambazo hazipaswi kuigwa na wanajamii wote ili walimu waweze kufanya kazi yao kwa weledi, ujuzi wa hali ya juu na tajriba komavu ya utoaji wa maarifa na ujuzi sahihi.

Imefikia wakati baadhi ya watu kusema, kazi ya Ualimu ni kwa wale waliopata alama ndogo darasani, na wengine husema baada ya mtu kukosa kazi nyingine hukimbilia kazi ya ualimu kama upenyo wa kupata chochote. Nikisema kutoka moyoni mwangu kwa kinywa changu tohara hili jambo si sahihi kabisa kwani taaluma ya ualimu ni kama taaluma nyingine na ifahamike kwamba TAALUMA YA UALIMU NI MAMA WA TAALUMA ZOTE.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom