Mchango wa Tabora Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika (1945 - 1961)

Mchango wa Tabora Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika (1945 - 1961)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MHADHARA: MCHANGO WA TABORA KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA (1945 - 1961)

Niko Tabora toka jana usiku.

Mwaliko wa Wazee wa CCM Tabora Kuadhimisha Kuzaliwa kwa CCM tarehe 5 February 1977.

Nimealikwa kuzungumza mchango wa Tabora katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mhadhara unafanyika Chuo Cha Uhazili leo asubuhi saa nne.

Katika historia hii ya Tabora kuna kitu muhimu.

1953 Gavana Edward Francis Twining alitoa Government Circular No. 5 kuwakumbusha watumishi wa serikali kutojihusisha na siasa.

TAA Tabora waliwatoa katika uongozi watumishi wa serikali wakachagua viongozi wapya.

Germano Pacha akachaguliwa Secretary Western Province na akatumwa TAA HQ New Street kwa TAA Act. President na Secretary Abdul Sykes kumtaarifu nia ya TAA Tabora kuunda chama cha siasa kudai uhuru.

Kipindi hiki ndicho Abdul Sykes na Hamza Mwapachu wanakabiliwa na suala la kuunda TANU na kumpata kiongozi.

Abdul Sykes akamwambia Germano Pacha kuwa wasubiri kuna mipango inafanyika na wataarifiwa.

Germano Pacha akajakuwa kati ya waasisi 17 wa TANU Julai 1954.
 
Hebu imalizie yote, wape pole Kwa kuting'indwa 3 na wekundu
 
Huyu Ustadhi asipomtia Ustadhi Sykes haoni raha.
 
Back
Top Bottom