SoC02 Mchango wa ufugaji nyuki katika kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo

SoC02 Mchango wa ufugaji nyuki katika kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

Mr beekeeper

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
1
Reaction score
2
UTANGULIZI

Ufugaji Nyuki ni sanaa na ni sayansi pia inayohusisha ukusanyaji , usimamizi na uongezaji wa makundi ya Nyuki kwa lengo la kuzalisha mazao ya mbalimbali ya Nyuki kama vile Asali, nta , gundi ya nyuki , sumu ya nyuki , maziwa ya nyuki , watoto wa nyuki n.k , lakini pia kufanya ustawi wa bayoanwai ya mimea mbalimbali kupitia uchavushaji. Hii ni moja ya sekta imara sana na inayokuwa kwa kasi duniani na yenye tija kwa mtu mwenye kipato cha chini, cha kati na cha juu. Ila kwa nchini kwetu bado ufugaji nyuki haujakuwa na tija kwenye masikio ya watanzania labda nikufungue masikio katika hili.

inbound2881265633517349613.jpg

Takwimu za nchi zenye misitu mikubwa barani afrika ambayo ni misitu asilia
1. Congo DRC ( 126.2 millioni hekta)
2. Angola ( 66.6 millioni hekta)
3. Tanzania ( 45.7 millioni hekta)
4. Zambia ( 44.8 millioni hekta)
5. Msumbiji ( 36.7 millioni hekta )
6. Gabon ( 23.5 millioni hekta )
7. Afrika ya kati ( 22.3 millioni hekta)
8. Congo ( 21.9 millioni hekta)
9. Nigeria ( 21.6 millioni hekta)
10. Cameroon ( 20.3 millioni hekta)
Chanzo: www.statista.com

inbound3354280591702627675.jpg


Hizo ni takwimu zinaonesha jinsi gani nchi yetu ni miongoni mwa mataifa kumi yenye misitu asilia mikubwa kulinganisha na mataifa mengine. Hii ni baraka kubwa kwetu sote kuitumia kujipatia kipato endelevu kwa utaratibu ambao nchi imetuwekea. Sasa unapogusia misitu mahali popote basi pacha wake ni Nyuki. Bila ya uwepo wa Nyuki baadhi ya miti inayounda hiyo misitu isingekuwepo hapa duniani kivipi ?na kwanini? nitakueleza kwa ufasaha huko mbele katika andiko hili.

Uhusiano wa misitu na ufugaji nyuki
Ufugaji nyuki unafanyika hususani katika maeneo mbalimbali ya misitu ambayo ni misitu ya vijiji, halmashauri na serikali kuu hapa nchini. Pia unaweza fuga nyuki katika shamba lako binafsi au bustani ambayo ipo nyumbani kwako. Watu wanaweza kustuka kusikia unaweza fuga maeneo karibu na makazi yetu . Ndio , inawezekana sababu ufugaji nyuki umegawanyika katika makundi mawaili nyuki wanaodunga( nyuki wakubwa) na nyuki wasiodunga( nyuki wadogo). Nyuki wasiodunga unaweza fuga maeneo ya nyumbani sababu hawana tabia ya kushambulia mtu pale wanapokumbana na changamoto mbalimbali. Misitu ndio nyumba ya mimea mbalimbali, mimea ndio inayozalisha chakula/malighafi kwa nyuki ambao ni chavua na mbochi.

inbound8560410002992991829.jpg



Ufugaji nyuki ni chachu ya kukua kwa uzalishaji katika sekta ya kilimo

Kilimo ni sekta mama katika uchumi wa mtanzania , ndiyo uti wa mgongo kwetu sote asilimia kubwa ya watanzania wanajihusisha na kilimo. Soko la chakula na mazao ya biashara ni kubwa sana duniani na bado linauhaba wa bidhaa hii ni fursa kwetu watanzania. Je tutafikaje huko kushindana na wengine duniani? Je, uzalishaji wetu unatupa hiyo fursa ya kuuza kiasi kikubwa cha mazao katika soko la kimataifa ? Je, mazao yetu yana ubora unaokidhi matakwa ya soko la kimataifa?. Nadhani, kila mtu atakuja na jibu lake lakini takwimu zinasemaje katika upande wa uzalishaji barani Afrika.

Takwimu za nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula barani Afrika.
1. Tunisia
2. Murutius
3. Morroco
4. Algeria
5. Egypt
6. Gabon
7. South Africa
8. Ghana
9. Senegal
10. Namibia
source : www. Consultancy.africa.com

Kupitia takwimu hizo inaonesha bado tupo nyuma katika uzalishaji wa mazao mbalimbali katika sekta ya kilimo kulinganisha na rasimali ardhi tulizopewa na Mungu .

inbound3462916887514549326.jpg


Sasa ni muda wa kutupia jicho kilimo chenye muunganiko na ufugaji nyuki.

Tanzania ni nchi mojawapo duniani yenye utajiri mkubwa wa makundi ya nyuki. Makundi ya nyuki wanaodunga na wasiodunga yanapita maeneo mbalimbali yakitafuta makazi mazuri na chakula ili waweze kuzaliana na kuendesha maisha yao hapa ndipo fursa ilipo subiri nikusogezee hii.

inbound790320414290410480.jpg



Uchavushaji wa mimea kupitia wadudu.

Hiki ni kitendo cha kibaiolojia kinachofanywa na wadudu mbalimbali kupitia kubeba mbegu za kiume kutoka sehemu me ya mmea kupeleka sehemu ke ya mmea kwaajili ya urutubishaji wa mbegu hadi kuwa tunda. Mfano wa wadudu hao nguli katika uchavushaji ni kipepeo, bito na nyuki. Nyuki ni mchavushaji hodari hususani katika mazao ya chakula yeye ndie anachavusha zaidi ya asimilia 85 ya mimea yote ya mazao ya chakula duniani mfano mpunga, uwele, ngano, mahindi n.k.


Faida za uchavushaji katika kilimo

1. Kuongeza kiwango cha uzalishaji mazao ya chakula na kibiashara

2. Kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za kilimo kama vile kutoa pesa kununua pembejeo na viwatirishi.

3. Kuzalisha mazao ambayo ni asili na yenye virutubisho asilia ambayo duniani yanatafutwa ,kwasababu mazao mengi yanatokana na matumizi ya mbolea za kisasa.

4. Kuzalisha matunda na mazao ya chakula kama vile tikiti, ndizi, mahindi, pasheni, mapera, machungwa, maembe kuwa yenye umbo kubwa lenye kuvutia mteja na mlaji.

5. Kuongeza kipato cha mkulima na kuweza kumudu gharama za maisha za sasa.

inbound2432594486291268038.jpg


Nini kifanyike nasi tuwe kinara ndani ya bara la Afrika na nje ya bara la Afrika.

Mosi , Tuwekeze zaidi katika kilimo cha uchavushaji . Serikali inapaswa kuongeza nguvu hususani katika bajeti ya wizara ya kilimo ili kuwezesha kununua vifaa maalum kama vile mizinga ya nyuki , makundi ya nyuki maalum kwa uchavushaji , Magari maalumu ya kubebea makundi, pia mavazi ya kujilinda mtoa huduma au mkulima dhidi ya makundi makali ya nyuki.
inbound5809352195712329818.jpg


Pili, Tuzalishe wataalam wengi wa elimu ya sayansi ya mazao na sayansi ya ufugaji nyuki. wataalam hawa ndio chachu ya maendeleo ya hii sekta ya kilimo na sekta ya ufugaji nyuki, ingawa katika hili serikali kupitia vyuo vyake Chuo kikuu cha Dar es salaam na Chuo kikuu cha Sokoine wameanza kuzalisha wataalam wa kutosha.

inbound1542933995959365840.jpg


Tatu, Jamii ipewe elimu jinsi ya kupunguza matumizi ya viwatirishi katika mashamba yao.kupitia vyombo vya habari na vipeperushi watu wahamasishwe kufanya kilimo hiki chenye tija.

inbound5808035066218897403.jpg


nne, Kuanzishwe mashamba darasa ya kilimo kinachotegemea uchavushaji.ili kujenga imani na hali ya kujiamini kwa wakulima lazima kuwe na mashamba ya kujifunzia aina hii ya kilimo kwani wanapaswa kujifunza kufuga na kufanya kilimo kwa wakati mmoja.

tano, kutolewe mikopo kwa wakulima wadogo na wajasiriamali watakao hitaji kufanya kilimo hiko.

sita , Kuundwe kitengo cha uchavushaji wa nyuki na wadudu wengine katika wizara ya kilimo.



SIFA ZA MAKUNDI YA NYUKI YANAYOFAA KUFANYA KILIMO CHA UCHAVUSHAJI.
1. Kundi la nyuki linapaswa kuwa ni kundi lenye Afya na imara ili kukabiliana na magonjwa na maadui.
2. Kundi la nyuki linapaswa kuwa na chakula cha kutosha kama vile asali, mbochi na chavua.
3. Kundi la nyuki linalofaa katika uchavushaji ni lile lenye idadi kubwa ya nyuki watumishi na malkia mwenye umri mdogo na mwenye uzalishaji mkubwa.


SIFA YA SHAMBA LINALOFAA KWA KILIMO CHENYE KUTEGEMEA UCHAVUSHAJI WA NYUKI.
1. Shamba linapaswa kuwa mbali na mashamba yanayotumia viwatirishi na kemikali mbalimbali katika ukuzaji wa mimea.
2. Shamba linapaswa kuwa karibu na cha chanzo cha maji sio zaidi ya kilometa 3 au kuwe na bwawa la maji.
3. Mkulima anapaswa kutotumia madawa ya kuuwa wadudu na magugu kwani kunaweza kuuwa makundi ya nyuki lakini kama itakuwa lazima basi atumie wakati wa asubuhi au jioni.

Andiko hili limeandikwa nami SUED JAFARI
Naomba kura yako na pia likes kama umependezwa na andiko langu.
 

Attachments

  • inbound7371436589248511488.jpg
    inbound7371436589248511488.jpg
    9.2 KB · Views: 15
Upvote 5
Back
Top Bottom