MCHANGO WA WAOKOTA TAKA REJESHI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA UCHUMI REJELEVU NCHINI TANZANIA
Imeandaliwa na Abdul-Aziz Carter.
Muhtasari
Waokota taka Rejeshi wanachukua jukumu muhimu katika kupambana na uchafuzi wa mazingira na kuchangia katika uchumi rejelevu kwa kuchakata na kutumia tena taka zinazoweza kurekebishwa. Ingawa mchango wao ni mkubwa, bado hawajatambuliwa kisheria nchini Tanzania, jambo linalozua changamoto za kiuchumi na kijamii. Ripoti ya UN Environment ya 2018 inatoa mapendekezo ya hatua zinazohitajika ili kukabiliana na changamoto hizi, ikiwemo kuweka mzigo wa gharama za usafishaji wa mazingira kwa wazalishaji wa plastiki. Utafiti wa Kamisheni ya Ulaya umeongeza msisitizo kwamba sekta ya uzalishaji wa plastiki inapaswa kubeba gharama za usafishaji wa mazingira, hatua itakayosaidia kudhibiti uchafuzi wa mazingira na kutoa unafuu kwa waokota taka Rejeshi.
Utangulizi
Utunzaji wa mazingira ni moja ya masuala muhimu duniani kote, na waokota taka Rejeshi wanachangia kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kwamba taka zinazoweza kuchakatwa zinarejeshwa katika mzunguko badala ya kutupwa. Hata hivyo, kutokana na kutoonekana kwa mchango wao katika sera za usimamizi wa taka nchini Tanzania, waokota taka Rejeshi wanakosa fursa za kiuchumi na kijamii.
Katika muktadha wa uchumi rejelevu, ambapo rasilimali zinachakatwa na kutumika tena, waokota taka Rejeshi ni sehemu muhimu ya mfumo wa utunzaji wa mazingira. Ripoti ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya 2019 na ile ya mwaka 2013 kutoka Shirika la Kazi Duniani zinaonyesha kwamba mchango wa waokota taka ni mkubwa katika kupunguza taka na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zinazochakatwa.
Hivyo, kuchangia katika uhifadhi wa rasilimali asili. Wanapochakata taka, wanapunguza hitaji la kutumia malighafi mpya, na kwa hiyo kulinda mazingira na kukuza uchumi rejelevu.
Mchango wa Waokota Taka Rejeshi katika Uchumi Rejelevu
Waokota taka Rejeshi wanachukua jukumu muhimu katika uchumi wa mzunguko, ambapo bidhaa huchakatwa na kurejeshwa katika mzunguko. Hivyo, mchango wao ni mkubwa katika kupunguza taka na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zinazochakatwa. Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) ya mwaka 2013 inaangazia mchango mkubwa wa waokota taka katika ukuaji wa uchumi rejelevu, hasa katika muktadha wa uchumi wa mzunguko na endelevu. Waokota taka wanachangia katika kupunguza athari za uchafuzi wa mazingira, kupunguza matumizi ya malighafi, na kuongeza kasi ya kurejesha bidhaa zilizozalishwa.
Changamoto Zinazowakabili Waokota Taka Tanzania
Waokota taka Rejeshi nchini Tanzania wanakutana na changamoto mbalimbali, kama vile:
1. Malipo Duni: Bei ya chupa za plastiki inayolipwa ni kidogo sana, kutoka shilingi 100 hadi 500 kwa kilo moja, ambayo ni kidogo ukilinganisha na juhudi wanazoweka.
2. Udanganyifu wa Vipimo na Mizani: Waokota taka wanakutana na udanganyifu kuhusu vipimo na mizani, ambapo mara nyingi wanalipwa kidogo kuliko kile wanachostahili.
3. Mtazamo Hasi wa Jamii: Waokota taka mara nyingi wanakutana na unyanyapaa wa kijamii, ambapo jamii inawaona kama watu wasio na hadhi au wahalifu.
4. Ukosefu wa Vifaa na Ulinzi: Waokota taka wanahitaji vifaa vya kujilinda kutokana na hatari za afya zinazotokana na mazingira ya kazi yao, lakini hawapati vifaa hivyo kwa urahisi.
Utafiti wa Mtandao wa Waokota Taka Rejeshi Dar es Salaam (MTAWADA) wa 2024 unaonyesha kwamba waokota taka katika jiji la Dar es Salaam hufanya kazi kwa saa 10 hadi 15 na kutembea kati ya kilometa 15 hadi 45, huku wakikusanya wastani wa kilo 10 kwa wanawake na wazee na kilo 25 kwa vijana. Kilo moja hununuliwa kwa shilingi 100 hadi 500, kulingana na msimu na utashi wa Mawakala.
Hatua za Kimataifa za Kutambua Mchango wa Waokota Taka
Nchi kama Brazil, India, Agentina na Kolombia zimeweka mifumo rasmi ya kutambua waokota taka Rejeshi:
Brazil: Waokota taka Rejeshi katika miji kama Sao Paulo na Belo Horizonte wanatambuliwa kupitia Sheria ya Kitaifa ya Usimamizi wa Taka Ngumu (PNRS), ambapo wanapata haki za kisheria na msaada.
India: Sheria ya Usimamizi wa Taka Ngumu ya mwaka 2016 inatambua waokota taka hasa katika miji ya Pune na Bangalore kama sehemu muhimu ya mfumo wa usimamizi wa taka.
Kolombia: Bogotá na Medellin imeanzisha mfumo wa kuwapa waokota taka vitambulisho rasmi, leseni, na haki za kufanya kazi kisheria.
Argentina: Buenos Aires imeanzisha mpango wa kuwajumuisha waokota taka katika mfumo wa usimamizi wa taka.
Mapendekezo kwa Serikali ya Tanzania:
1. Kutambua Rasmi Waokota Taka Rejeshi: Serikali inapaswa kuweka sera zinazowatambua waokota taka kama sehemu muhimu ya mfumo wa usimamizi wa taka.
2. Kuweka Bei Elekezi ya Chupa za Plastiki: Serikali inapaswa kuweka bei elekezi kwa chupa za plastiki ili kuboresha mapato ya waokota taka.
3. Kusimamia Vipimo na Mizani: Serikali inapaswa kuhakikisha utekelezaji wa sheria za vipimo na mizani ili kuwalinda waokota taka dhidi ya unyonyaji.
4. Kutoa Vifaa vya Kujilinda: Wazalishaji wa plastiki wanapaswa kuwajibika kutoa vifaa vya usalama kwa waokota taka.
5. Bima ya Afya: Waokota taka wanapaswa kupatiwa bima ya afya bure kutokana na mazingira hatarishi wanayofanyia kazi.
6. Kudhibiti Chupa za Plastiki za Rangi: Kanuni za kudhibiti chupa za plastiki za rangi, kama ilivyofanyika kwa mifuko ya plastiki, zinahitajika.
Hitimisho
Ripoti ya Haki ya Mazingira Duniani (GEO-6) ya Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) iliyochapishwa mwaka 2019 inathibitisha mchango wa waokota taka Rejeshi katika utunzaji wa mazingira.
Waokota taka Rejeshi wanachangia kwa kiwango kikubwa katika uhifadhi wa mazingira na uchumi rejelevu, lakini bado wanakutana na changamoto nyingi. Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua za haraka kutambua mchango wao na kuboresha mazingira ya kazi yao.
Kama ilivyofanyika katika nchi nyingine, hatua za kutambua na kusaidia waokota taka Rejeshi zitachangia katika mafanikio ya maendeleo endelevu na uhifadhi bora wa mazingira. Serikali ya Tanzania inapaswa kuitambua na kuirasimisha kazi ya uokotaji taka Rejeshi.