World Logistics Company
Member
- Jun 1, 2021
- 99
- 104
Wakati dunia bado inahangaika na janga la corona au UVIKO19, nasi tumeona tutoe mchango wetu kwa wanaotafuta riziki kupitia biashara zao hususan wale wanaofuata bidhaa zao huko China, Uingereza, Uarabuni na mataifa mengine.
Siku hizi kusafiri imekuwa shida sana, shida zaidi ni kuagiza na kufuata mzigo nje ya Tanzania. Wajasiriamali wanakutana na vikwazo pale wanapotaka kufuata mzigo na hawajachanja chanjo ya corona. Hii imekwamisha biashara za watu wengi achilia mbali kuchelewesha huduma katika sekta mbalimbali.
MCHANGO WETU NI UPI?
Ili kulinda afya za watanzania na kunusuru biashara za wajasiriamali na sekta nyingine zinazoagiza na kufuata mizigo nje ya nchi, sasa tutakuwa tunafuata mizigo na bidhaa popote pale nje ya nchi na kuwasaidia kusafirisha kuja nchini. Hii itaepusha usumbufu wa safari, gharama pamoja na kutolazimisha wale wasiotaka kuchoma chanjo kwa sasa, kuchoma kwa sababu tu za kibiashara.
Tunaamini kwa kufanya hivi tutaweza kusaidia kuchochea uchumi na kuepusha vifo vya biashara na ucheleweshaji wa huduma. Huu utakuwa ni mchango wetu na tunaamini unaendana na dira ya serikali katika kuinua uchumi wa nchi yetu.
Tunakaribisha maswali, maoni na ushauri.