Mchawi

Mchawi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Alitokea mchawi, kuwaroga watu hawa.
akawapa ukiziwi, na magonjwa ya'so dawa.
kawafanya wawe kiwi, ndege wasio na mbawa.
mchawi alipania, kuwatesa si kuua.

kawaroga mashujaa, kafanya wawe wanyonge.
Kawaroga wenye njaa, kwa uchawi wa matonge.
karoga saa na taa, kuvizuzua viringe.
mchawi amewaweza, wenyewe walijiuza.

kawatupia majini, mengi yasiyo idadi.
akawatenda kihuni, hata kipofu shahidi.
wanaenda hawaoni, karoga kichwa na bodi.
mchawi alipania, kuwatesa si kuua.


kawafisha kiuwongo, kawafanya mizukule.
amewaroga ubongo, kwa wao akili nywele.
karoga jino na pengo, vilivyomeng'enywa wale.
mchawi alipania, kuwatesa si kuua.

MOLA PONYA WALIOROGWA ...!
MOLA WARUDISHE MASHUJAA WETU.
 
Back
Top Bottom