Mchekeshaji Dkt. Michael Usi aapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Malawi kufuatia kifo cha Saulos Chilima

Mchekeshaji Dkt. Michael Usi aapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Malawi kufuatia kifo cha Saulos Chilima

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Vice-President-DR.-Micheal-Usi-jpg.jpg
Dkt. Michael Usi ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Malawi katika hafla iliyofanyika katika Bunge la nchi hiyo mjini Lilongwe. Mchekeshaji huyo aliyebadilika kuwa mwanasiasa anachukua nafasi ya Saulos Chilima, ambaye alifariki katika ajali ya ndege mapema mwezi huu.

Dkt. Usi ameahidi kuheshimu kumbukumbu ya mtangulizi wake na kumshukuru Rais Lazarus Chakwera kwa kumuamini anapochukua nafasi yake kama Makamu wa Rais katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Uteuzi wake umewagawa Wamalawi huku baadhi yao waki-share vipande vya video zake za uchekeshaji kwenye mitandao ya kijamii na kuhoji kama anachukulia jukumu hilo la juu kwa uzito wa kutosha. Hata hivyo, wengine wamemsifu Rais Chakwera kwa kumteua Naibu wa chama cha Chilima na kuheshimu roho ya muungano kati ya vyama vyao viwili.

Usi amekuwa kipenzi kwenye vipindi vya vichekesho vya redio na televisheni vya kitaifa nchini Malawi kwa zaidi ya miongo miwili, na kumfanya kuwa mmoja wa watu maarufu sana nchini, huku wasaidizi wake wakisema alikuwa akirekodi kipindi cha vichekesho kitakachorushwa kwenye televisheni wiki iliyopita.

---
Dr. Michael Usi, 55, has been sworn in as Malawi’s Vice President at a ceremony held in the country’s Parliament in Lilongwe. The comedian-turned-politician replaces Saulos Chilima, who died in a plane crash earlier this month.

Saying he has accepted the role with a mixture of sadness and gratitude, Dr. Usi has promised to honor his predecessor’s memory and thanked President Lazarus Chakwera for believing in him as he takes up his position as Vice President in the power-sharing government.

His appointment has left Malawians divided. Some have been sharing clips of his acting career on social media and questioning whether he is serious enough to take up such a senior role. Others, however, have praised President Chakwera for appointing Chilima’s party deputy and honoring the spirit of the alliance between their two parties.

Usi has been a staple on national radio and television comedy shows in Malawi for more than two decades, making him one of the most recognizable local celebrities in the country, with his aides saying he was filming a comedy episode to be aired on TV as recently as last week.

Pia soma TANZIA - UPDATE: Makamu wa Rais wa Malawi afariki katika ajali ya Ndege
 
Napiga picha Kingwendu akiapishwa...!!! Ana Hali kama Raia wengine kubeba majukumu haya.
 
Hizi ajali za ndege kwa viongozi nahisi maboss huwa wana mikono yao
 
Back
Top Bottom