Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kijana Frank Patrick (Mchekeshaji wa Mtandaoni) maarufu Kama Molingo (17) Mkazi wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo December 10,2024 akiwa nyumbani kwao Chato ambako alikuwa akiuguzwa na Mama yake mzazi.
Rafiki yake ambaye alikuwa akiishi nae na kumrekodi vichekesho vyake Mudi Msomali ameiambia Ayo TV kuwa Molingo alikuwa anaugua mara kwa mara na chanzo cha ugonjwa bado hakijajulikana huku akisema muda mwingine alikuwa anavimba mwili na kuishiwa damu Mwilini.
"Molingo Bwana alikuwa anaumwa maradhi hayaeleweki kila wanachopima hawaoni kitu kwahiyo ndio hivyo mara ya kwanza walihisi labda ni Sickle cel (selimundu) walipima akawa yuko sawa wakawa wanahisi bandama mara moyo yaani kiufupi anarudi kwao hatukujua shida hasa ni nini"
"Madaktari walishauri mpelekeni kwao kwahiyo nahisi walikuwa wameshaona ila Mimi tu kama Mtu mzima nilijiongeza nikamwambia Anna itakuwa labda wameona mbali wanashauri mumrudishe kwao kwahiyo ndio hivyo alikuwa anavimba tuu mwili anaishiwa damu mara kwa mara"