Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kupanga ratiba ya uzinduzi wa miradi mbalimbali iliyosalia kwa kushirikisha wabunge.
Akizungumzia suala hilo, Mchengerwa amesema “Sasa kwa kuwa tunayo miradi mingi ambayo bado haijafunguliwa, wabunge hawa wamefanya kazi nzuri. Nitumie fursa hii kuwaelekeza wakuu wa mikoa, wilaya hapa, wakurugenzi wa halmashauri sasa kuwapangia wabunge hawa miradi yote ambayo haijazinduliwa. Waende mara moja katika majimbo yetu yote mia mbili kumi na tano.
Wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wakurugenzi waandae utaratibu uleule kama nakwenda waziri kiongozi wa juu kabisa waende wabunge wa kuzindua miradi hii kwa sababu wabunge hawa ndiyo waliosemea miradi hii ikashuka kule kwenye majimbo yetu. Wabunge hawa. Wamefanya kazi kubwa na kazi nzuri sana”.
Mchengerwa alitoa agizo hilo leo, Jumanne, Februari 11, 2025, wakati akichangia hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, katika kikao kilichofanyika bungeni jijini Dodoma
Tunachohitaji ni upatikanaji au utekelezwaji wa hiyo miradi na sio uzinduzi pekee. Wanazindua mradi mfano wa maji, zahanati/ hospitali; baada ya uzinduzi huduma hazipatikani