Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Wakienda kukata rufaa wanakuta ofisi zimefungwa! Imekuwa kama mchezo wa paka na panya!
====
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema wagombea wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao hawakutendewa haki, bado wanayo nafasi ya kukata rufaa.
Kupata nyuzi kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mchengerwa amesema rufaa hizo zinazokatwa ngazi ya wilaya zinapaswa kukatwa na wagombea wenyewe na si vyama vya siasa. Muda wa rufaa umeanza Novemba 10 hadi kesho Jumatano, Novemba 13, 2024.
Waziri huyo amesema hayo leo Jumanne, Novemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam katika semina ya wahariri kuhusu Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
"Muda wa kukata rufaa bado upo, watu wakate rufaa wasikae majumbani na kuviachia vyama vyao, rufaa inakatwa na mgombea. Kwa hiyo wale ambao wanaona hawajatendewa haki wakate rufaa sasa," amesema.
Aidha, Mchengerwa amesema uchaguzi huo utakaofanyika Jumatano ya Novemba 27, 2024 umeshirikisha vyama vyote 19.