Mchengerwa na Nape mko serious kuhusu mpira wa miguu nchini?

Mchengerwa na Nape mko serious kuhusu mpira wa miguu nchini?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Nimemsikia Nape anasema serikali inataka kuandaa Afcon...

Baadae nikamsikia Mchengerwa anasema tunaenda kombe la Dunia mwaka 2030...swali la kuwauliza hawa ndugu zetu wako serious?...

Kama wako serious mbona hatuoni hata hatua za mwanzo za maandalizi?..

Hatua ya Kwanza ilikuwa kuunda committee ya maandalizi na ushauri Kwa serikali...Binafsi ningempa hiyo nafasi Leodgar Tenga aje na timu yake...unaweza ongeza kina GSM na Mo humo na kampuni ambazo serikali ina hisa zikawepo pia...NMB. NBC n.k...na wataalam wengine...

Hatua ya pili ni lazima nchi iandae mashindano ya level ndogo lakini ya kimataifa kama njia ya kujipima...mfano world cup under 17... Afcon women....au world intercontinental championship..

Au wold club championship...n.k...

Halafu ndo mnakuja kuandaa Afcon ..mkiwa mmeshajipima.....

Ili kuandaa Afcon mnahitaji hata miaka mitano au zaidi ya maandalizi......

Lakini kama lengo ni kutangaza nchi why Taifa lisiandae events za kimataifa mbalimbali ambazo ni nafuu Kwa gharama lakini impacts yake ni ya kimataifa kama maandalizi kuelekea kuandaa hiyo Afcon?
Why not Miss world?....why not Miss universe?..events hizi zitatangaza nchi dunia nzima ....Kwa gharama nafuu pia....kuliko kukurupuka moja Kwa moja mseme tunaenda andaa Afcon wakati hatujawahi kujipima?
 
Hili wazo la kuhost mashindano makubwa binafsi nimekuwa nalo kitambo Sana, kama tutakuwa na nia thabiti tutaweza The Boss

Kama unawasi na Gharama sidhani kama tunaweza kushindwa. Tuna viwanja zaidi ya vitano ambavyo vinahitaji Minor repairs/rehabilitations hasa kupanda nyasi bandia n.k.

Kwahiyo kwa mashindano kama ya AfriCON tunaweza bila kuhitaji usaidizi mkubwa lakini kwa Kombe la Dunia tunahitaji walau kuungana na Wenzetu kadhaa.

Suala la Amani yetu ya Nchi inaweza kuturahisishia kwenye kupewa uwenyeji.

Kama Serikali ipo serious na hilo, waharakishe huo mchakato na wadau wapewe taarifa mapema ili Mahoteli yajengwe mapema.

Hakuna mchezo wenye Ushawishi Mkubwa Duniani kwa Sasa Kama Mpira wa Miguu.

Huko kwenye Mashindano ya Umiss hakuna mvuto Sana, we Imagine fainali za World Cup zilivyo na amsha, hadi huku Vijijini watu wanaangalia hata kwa kutumia Majenereta lakini ingekuwa huo Umiss wengine hata tusingekuwa wafatiliaji.
 
Hili wazo la kuhost mashindano makubwa binafsi nimekuwa nalo kitambo Sana, kama tutakuwa na nia thabiti tutaweza...
Miss world na miss universe inatazamwa huko duniani... kwahiyo lengo la kutangaza nchi linakuwa limefikiwa
 
Serikali haina hela ya kuandaa Afcon
 
Miss world na miss universe inatazamwa huko duniani... kwahiyo lengo la kutangaza nchi linakuwa limefikiwa
Upo sahihi Mkuu!

Ila kwenye hili la kuomba uwenyeji wa Kombe la AfriCON na World Cup, kama tutajipanga vizuri na kutumia Ushawishi wa Madam President nadhani 2030 tunaweza kupewa.

Muhimu tungeongeza Bajeti ya Wizara ya Michezo na Burudani ili tufanye matengenezo ya hivyo viwanja.

Tukifanya maintenance ya Uwanja wa Uhuru, Lupaso, Mabatini Pwani, Uwanja Manungu -Morogoro, Jamhuri Dodoma tungeweza kuhost kabisa.

Hizo fainali zitaongeza Mapato kupitia Utalii, Viingilio, Hotel/Lodges n.k.
Hata Wakina Shishi Food watapiga Pesa
 
Tujitahidi ili tuache kulalamikia wenzetu wakifanikiwa na kuanza kufurahia mafanikio yao kwa namna wanayoipenda.
 
Haya matamko yakitekelezwa na serikali ya ccm mimi nitajiuzulu uraia wa Tanzania.
 
Upo sahihi Mkuu!

Ila kwenye hili la kuomba uwenyeji wa Kombe la AfriCON na World Cup, kama tutajipanga vizuri na kutumia Ushawishi wa Madam President nadhani 2030 tunaweza kupewa.

Muhimu tungeongeza Bajeti ya Wizara ya Michezo na Burudani ili tufanye matengenezo ya hivyo viwanja.

Tukifanya maintenance ya Uwanja wa Uhuru, Lupaso, Mabatini Pwani, Uwanja Manungu -Morogoro, Jamhuri Dodoma tungeweza kuhost kabisa.

Hizo fainali zitaongeza Mapato kupitia Utalii, Viingilio, Hotel/Lodges n.k.
Hata Wakina Shishi Food watapiga Pesa
Hivi nyie mko siriasi kabisa mnajadili kuhusu Tz kuandaa kombe la dunia?
Au mpo mnafanya vichekesho hapa?

Labda kama ni Africon.
 
Mkuu ninaamini unatania tu.
 
Hivi nyie mko siriasi kabisa mnajadili kuhusu Tz kuandaa kombe la dunia?
Au mpo mnafanya vichekesho hapa?

Labda kama ni Africon.
Afcon I believe
 
Hamna aliye serious hapo.

Hamna anayeweza kufanikisha lolote hapo.

Ni kujichosha kuweka matumaini kwenye hivyo vichwa hapo.
 
Hamna aliye serious hapo.

Hamna anayeweza kufanikisha lolote hapo.

Ni kujichosha kuweka matumaini kwenye hivyo vichwa hapo.

Labda wapo serious...... ingawa ni tabu kuwaamini
 
Mkuu ninaamini unatania tu.
Wakati mwingine ni suala la vipaumbulele tu, hakuna mahali penye hela kama kwenye entertainment and sports. Imagine saivi Qatar wanapiga hela kiasi gani?

Kama hatuwezi na tuna Nia, tunaweza kuandaa kwa ushirikiano wa baadhi ya majirani zetu hapa EAC
 
wanajisemea tu hao. unafahamu maana halisi ya siasa ya Tanzania?

maana halisi ya siasa ya Tanzania ni kusema pasipo vitendo kwa ajili ya kuwafurahisha watu au kutuliza jambo fulani.
 
Back
Top Bottom