Mchengerwa: Tanzania kushiriki Kombe la Dunia 2030

Tyrone Kaijage

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
1,617
Reaction score
3,405
Ni ripoti ya Clouds Media na haya ni sehemu ya maneno yaliyosemwa na Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ukisikiliza kwa kina maelezo yake utaona ni yale yale kama ya lile garimoshi la umeme tuli linalolalamikiwa , upande wangu naona kuwa bado viongozi WaTanzania hawajakubali kuwa kuna vitu havitaki porojo za siasa bali ni mipango ya kweli.

Popote kwenye ndoto kubwa ni lazima kuwe na mgawanyo wa hatua mbali mbali za kuifikia,tusione Morocco wanaupiga vile tukadhani ni rahisi kufika pale, anyway basi tuwe na angalau na mipango hata ya kufika mbili mfululizo AFCON kwanza.

Tuna mipango gani ya uvunaji wachezaji na vipaji, sambamba na mifumo sahihi ya uendeshaji mpira wetu kuanzia mtaan chandimu, vilabu mpaka taifa.

Uvunaji wachezaji,inaweza kuwa kwa kuanzish academy au kwa kuanzisha sera za ku push michezo kuanzia mtaani, mfano siku hizi ukipita mitaani hata kukuta maeneo ya wazi ya michezo kwa watoto ni adimu.

Kupitisha sera za uraia pacha,tuvute vijana wa Kibongo walizoliwa nje na wenye exposure kuja kuongeza nguvu.

Mamlaka ziwe na watu wa michezo halisi sio wanasiasa wa michezo.

Sera ziwe za Wizara na ndio ziwe misingi ya dira ya Taifa, isiwe ya Waziri maana kesho huyo Waziri anaweza asiwepo hapo ukamkuta Wizara ya Afya huko…

Tyrone KG
 
Ukweli ni kwamba Tanzania hakuna vipaji vya mpira wa miguu, tunalazimisha tu.

Tuwekeze zaidi kwenye Riadha na Masumbwi tutafika mbali.
 
Ukweli ni kwamba TZ hakuna vipaji vya mpira wa miguu, tunalazimisha tu.

Tuwekeze zaidi kwenye Riadha tutafika mbali.
We acha hizo yule kocha wa saudi arabia alitaka kuja kufundisha Tanzania kipindi hicho baada ya kufanya tafiti na kugundua afrika mashariki hakuna sehemu yenye vipaji kama Tanzania hata kocha wa singida big stars alishasema hilo hata mwinyi zahera kila siku anasema ila sasa kuviendeleza ndo tatizo tunaruhusu wanasiasa waingie kwenye michezo kosa kubwa sana hilo.
 
Huyo mbunge huku kwetu Rufiji kumemshinda anawaza ambayo hayapo hata katika ilani ya CCM ya Joseph Makamba.
 
Ukweli ni kwamba TZ hakuna vipaji vya mpira wa miguu, tunalazimisha tu.

Tuwekeze zaidi kwenye Riadha tutafika mbali.

Miaka fulani tulikuwa tunaburuza sana kwenye masumbwi enzi za kina snake boy Matumla, ila ukiangalia ndio vile vile talent made in Mtaani as a nation hakuna mipango….

Hii ndio inamfanya hata Mwakinyo huwa ana mind sana the way alivyo raise na msaada mipango ya hawa wanasiasa.
 
Ni ripoti ya Clouds Media na haya ni sehemu ya maneno yaliyosemwa na Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo...
Hata tukipewa nafasi ya timu kumi hyo 2030 bado tz hatutafuzu, kama uganda anatupasua kila siku, tutaweza kupambana na kina moroco na senegal, wakati sisi tunajitia moyo nchi nyngine zinaweka mipango serious ya kufuzu na kufanya vizuri kombe la dunia.

Mi nadhan tuendelee kupambana na maadui wetu watatu ,umaskini, maradhi na UJINGA, uliozalisha maadui wapya ambao ni UFISADI na UCHAWA.

Mpira tucheze kwa starehe lakini tusipeane malengo yoyote, hasa kwa timu za taifa.
 

Yes adui “UJINGA” kashazaa, na kujukuu kwa kuwa mwanawe “UCHAWA” anazaa kundi la “UPINDE”
 
afrika mashariki hakuna sehemu yenye vipaji kama Tanzania
Kweli ila ukigundulika una kipaji km huna mtu wa kukupush ukakionyesha kikafika mbali ni sawa na bure tu, kuna academy nyingi za watu wenye vipaji ila sio za bure lazima ugharamikie matunzo ya kwenye academy (ni za kulipia km vyuo au shule za private) na wenye academy ni watu binafsi sio Serikali

Hizo gharama za academy wenye vipaji hawawezi kuzimudu. Wanaishia kufa na vipaji vyao tu.

Mwakinyo was lucky to be where he is na hakufika yeye mwenyewe behind him kuna watu ila sio Serikali. Serikali ilimtambua baada tu ya kufanikiwa Uingereza before that hawakua wakimjua zaidi ya juhudi zake binafsi na waliompambania kufika alipofika.
 
Inatosha sana kushiriki mashinfano ya Kombe la Dunia la Walemavu, na pia Wanawake chini ya miaka 17.

Kuhusu Kombe la Dunia la Wanaume; tudahau iwapo tutaendelea na hizi sera za CCM, za kukataa uraia pacha, kutokuwekeza kwa vitendo kwenye sekta ya michezo! Na hasa kwenye soka la vijana, kuanzisha mitaala ya michezo mashuleni, nk. viwanja vya wananchi kuendelea kumilikiwa na CCM, nk.
 
Kwahiyo nawewe ukaamini hizo stori?.Kipaji hakijifichi ndugu.ukishakua nacho kitajionyesha tu na kitakubeba popote pale.Kipaji ni karama inayotoka kwa Mungu mwenyewe.Itoshe kusema tuna vipaji vya kawaida ambavyo kila sehemu vipo zaidi ya hapo ni siasa na stori zakujifariji.
 
Tatizo hufuatilii mambo ww vipaji vipo ila hela ndo inarudisha watu nyuma kuna team ya vijana ilifuzu mashindano ya kimataifa sasa unaambiwa siku ya safari pale airport team inataka kuondoka hakuna hata mchezaji mmoja aliyekuwepo awali wote wapya na ni watoto wa vigogo kocha akagoma kuondoka nao ikabidi wafanyiwe mpango wale wa mwanzoni japokuwa hawakuwa wote ila walikuja baadhii tu ikabidi kishingo upande tu kocha akaondoka nae yaani kiufupi ngozi nyeusi ni shida nasikia huko CAMEROON kwa etoo ilikuwa ili uitwe national team ni lazima ulipe hela ili uitwe na kuanza kila mechi halafu kwenye national team akamuweka rafiki yake ili ampangie kikosi maana kamkamata masikio kiufupi soka la Africa lote ni uozo bila hela utoboi baba yake mbape alishasema alimpeleka mwanae kwenye academy za CAMEROON wakataka hela akaenda nae France wakamchukua bado mpaka hapo una mashaka na vipaji tu tatizo hela bila hela hakuna sehemu yoyote utatoboa nchi hii.
 
Inawezekana 2030 kusiwe hata na nchi inaitwa Tanzania...maana tuliambiwa na Ndugai tukiendelea kukopa kopa tutauzwa🐒
 
Hapo kwenye Ufisadi na Uchawa umemsahau na Chura nae.
Holi Taifa ni bora lipigwe nyukilia tu, tukifa wote wenda kikazaliwa kizazi chenye faida.
 
Sio kwa nia mbaya Ila kwa tulivyooza na tunaendelea kushikilia hii structure iliyooza tukifuzu niite mbwa nimekaa pale😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…