Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nilipata stori kwenye kijiwe kimoja, kuna mwanamke alikuwa ameolewa na wakabahatika kuwa na watoto. Kwa bahati mbaya mumewe akahamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine, huku nyuma akaamua kuiacha familia ya watoto na mke ili akishajipanga huko ugenini, aje awachukue.
Baada ya miezi kadhaa kupita, mumewe akawa ameshajipanga vizuri, ikabidi amuombe mkewe na watoto wamfuate huko alipo; cha kushangaza mkewe alikataa.
kukataa kwa mkewe huko, kulitokana na huyo mkewe kuanzisha mahusiano mapya pamoja na kuishi na mwanaume mwingine (mchepuko). Mumewe hajui hili wala lile, alipopata nafasi ilibidi arudi nyumbani kuja kuangalia familia.
Ile kupita pita njiani, ndipo mchepuko ukamuona mume wa yule mwanamke; matokeo yake, mchepuko ulirudi nyumbani, na inavyoonokena kulikuwa na majibizano ya hapa na pale, na matokeo yake akachukua kitu kizito na kumpiga mke wa mwenzie, mpaka umauti ukamfika. Bahati nzuri, hayo yote yakitokea, mtoto mdogo alikuwepo ndio aliyekuwa akitoa ushahidi.
Cha kujifunza, unapokuwa na mchepuko msikolezane mpaka kupoteza ufahamu wa kufikiri.