Mchezaji gani unamkubali kwenye kupiga penati?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Jioni moja ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba Vs FC Platnum, mechi ya marudiano ya Klabu Bingwa Afrika, matokeo yakiwa ni 0-0 Simba wanafanikiwa kupata penati, wachezaji wa Platnum wanashinikiza kugomea mechi lakini baadae wanakubali kurejea uwanjani, wanajaribu kumgasi mpigaji wa penati ili kumuondoa mchezoni na lengo likiwa akose penati ile.

Lakini katika utulivu wa hali ya juu, Erasto Edward Nyoni anafunga penati ile na kuwarudisha Simba mchezoni na hatimaye kufuzu hatua ya makundi.

Ni wachezaji wachache sana wenye utulivu mkubwa linapokuja swala la kupiga penati hasa penati ya maamuzi au penati muhimu.

Mchezaji gani unaamini ni bora sana kwenye upigaji wa penati?

Karibuni...
 
Katika ligi ya VPL na nchi ya Tanzania kwa ujumla hakuna mpiga penati mzuri zaidi ya Nyoni, kwakweli sijawahi kuona au kuskia kakosa penati, na Hilo jambo inaonekana ata ndani ya team ya Simba linajuliakana ndomana baada ya kupata penati mchezaji kama Chama anaenda kumpa mpira Nyoni apige ni wazi anajua uwezo wake, refer mechi ya Uganda vs Tanzania tumepata penati samatta anaenda kumpa Nyoni, kwahiyo chaguo namba 1 ni Nyoni na nje ya Tanzania ni Cr7
 
Charles Nyoni[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Mechi ya Simba na kagera sugar dakk ya 89 bila bila mara ghafla kagera akapata penati, mashabiki wa Simba walivoona SALUM KANONI kaenda kuchukua mpira akapige penati ndipo historia ya kung'oa viti ilipoanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…