Mchezaji kusajili na timu nje ya muda wa dirisha la usajili

Payrol

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2018
Posts
2,286
Reaction score
3,082
Naomba nisaidieni hii kisheria za mpira inakuaje, Dirisha dogo la usajili Ligi kuu Tanzania bara liliisha tarehe 15 Jan 2020, lakini Morrison aliingia nchini 17 Jan 2020.

Kwa tarh hiyo inamaana kua Morison alisajiliwa nje ya muda wa Dirisha la usajili, maana kabla ya mchezaji kusajili kuna kumuombea vibali vya kazi ndipo asalijiliwe kwenye mfumo.

Kama ikajulikana Yanga walimsajili nje ya muda wa usajili. Je, Yanga wanaweza wakapokonywa point zote za mechi alizocheza Morrison au sheria inasemaje?
 
TFF hawakuliona hilo mwanzo? Kama waliliona kwanini hawakuchukua hatua mpaka lilipoibuka hili?
kuliona au kutoliona hakuhalalishi makosa kuna kanuni ambazo zinaongoza soka kwa sheria za chama husika lakini kuna sheria ambazo zitaibana tff ikibainika ilifanya uzembe kwa kifupi tff wamekuwa wakiziogopa hivi vilabu viwili pale vinavyovunja sheria
 
Conclusively tunaweza kusema TFF watafanya maamuzi katika sakata lililopo bila kugukua makaburi kwasababu yatawanukia na wao.
 
Conclusively tunaweza kusema TFF watafanya maamuzi katika sakata lililopo bila kugukua makaburi kwasababu yatawanukia na wao.
sasa hivi zinapambana timu kubwa, ni rahisi kufukia makaburi kama timu kubwa inapambana na timu ndogo.
 
Morrison kaja tarehe 17 na usajili ulifungwa tarehe 15.

1. Je mkataba baina ya Yanga na Morrison ulifanyika baada ya Morrison kufika Tanzania au walisainishana kwa njia za kimtandao kabla hata ya kuja hapa Tanzania?

2. Je Yanga waliwasilisha jina la Morrison kuwa ni mchezaji wao kabla ya dirisha kufungwa au baada ya dirisha kufungwa?

3. Je huo mkataba waliosainishana unasema kuwa Morrison amepewa kandarasi ya muda gani? Maana hapa ndipo tatizo lilipoanzia na kupelekea kufikia malumbano baina ya Yanga na Morrison
 
Ko unataka kusema Yanga walimuombea mchezaji kibali cha kufanya kazi nchini kabla ya mchezaji kutua nchini?
 
Vipi kama morrison alisaini mkataba akiwa ghana maana eng anasema alimtoa morrison ghana kijijini huko
 
Ko unataka kusema Yanga walimuombea mchezaji kibali cha kufanya kazi nchini kabla ya mchezaji kutua nchini?
Nauliza maswali ili nijue swala lilivyo. Nawewe unakuja unaniuliza swali.
 
kuna mpumafu mmoja anaitwa magori ndiye anaye wadanganya na kuwachanganya mikia fc

Mpe heshima yake bwana, mtu mwenye cv kubwa kama yule Mpaka Rais wa inchi alimwamini unamwitaje mpumbavu?
 
Nauliza maswali ili nijue swala lilivyo. Nawewe unakuja unaniuliza swali.
Sikujua ka unauliza swali, mwenyewe ndo maana nimeuliza ili nipate ufafanuzi kwa wanaolijua vzr sakata hili
 
Mpe heshima yake bwana, mtu mwenye cv kubwa kama yule Mpaka Rais wa inchi alimwamini unamwitaje mpumbavu?
huyu ni kanjanja tuu, uki re call memory yako vizuri hata raisi alimfukuza kazi a.k.a 'kumtumbua' kutoka kule NSSF alipokuwa mkurugezi yeye na lile jizi linguine lililo pelekwa ubalozin, hivyo huyo jamaa ana sifa nyingine ya 'ujizi'
 
Inshu hapa ni huo mkataba wa kwanza wa miezi 6,ulikuwa halali,? kutokana na kuonekana kuwa aliingia nchini tarehe 17,wakati dirisha lilifungwa 15? Kama mkataba huo ulikuwa batili, basi hata huo wa miaka miwili uliongezwa juu ya huo batili nao, utakuwa batili tu!!
 
huyu ni kanjanja tuu, uki re call memory yako vizuri hata raisi alimfukuza kazi a.k.a 'kumtumbua' kutoka kule NSSF alipokuwa mkurugezi yeye na lile jizi linguine lililo pelekwa ubalozin, hivyo huyo jamaa ana sifa nyingine ya 'ujizi'

Wivu tu
 
Kwa maana hiyo Yanga walimchezesha Morisson bila mkataba halali je hili nalo ni kosa la nani ??
 
4. Je TFF hawakuongeza muda wa dirisha la usajili baaada ya hiyo 15 ufika mwisho?
 
TFF hawakuliona hilo mwanzo? Kama waliliona kwanini hawakuchukua hatua mpaka lilipoibuka hili?
Mwizi asipoonekana wakati anaiba vitu supermarket, haihalalishi tendo la kuiba. Baada ya kureplay video iliyorekodiwa na security camera na kumuona mwizi akifanya yake, adhabu inamstahili, hata kama awali walinzi hawakugundua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…