real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Kiungo wa Real Madrid, Luka Modric anakabiliwa na mashtaka nchini mwake, Croatia ambayo huenda akahukumiwa kifungo jela.
Mwanasheria Mkuu nchini humo alithibitisha mchezaji huyo kujihusisha na ukwepaji kodi pamoja na masuala ya rushwa kwenye kesi ya rais wa zamani wa Dinamo Zagreb, Zdravko Mamic.
Kutokana na makosa ya ukwepaji kodi na kutoa rushwa, Mamic na wenzake watano walihukumiwa mwaka 2015 kutokana na bonasi waliyopiga baada ya kuuza wachezaji huku miongoni mwa wachezaji waliouzwa walikuwa ni Modric akitokea Dinamo kwenda Tottenham 2008.
Hata hivyo baada ya uchunguzi wa kina imebainika, Modric (32) alitoa ushahidi wa uongo tofauti na ule aliotoa mwaka 2015. Kesi ya aina hiyo mshatkiwa anaweza kukabiliwa na kifungo cha miezi sita hadi miaka miatano kwa sharia za Croatia.
Chanzo: Mwananchi