Mchezaji Raia wa Ghana Raphael Dwamena Aanguka na Kufariki Uwanjani

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Raphael Dwamena amedondoka leo hii ghafla uwanjani na kupoteza maisha, wakati timu take ya KF Egnatia ikicheza dhidi ya Albania ikiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Partizan.

Mchezaji huyo mara baada ya kudondoka alipatiwa huduma ya kwanza uwanjani hapo na kukimbizwa hospital lakini ilishindikana kuokoa maisha yake na akapoteza maisha.

Dwanema mwenye miaka 28, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambao ndiyo chanzo cha kifo chake.

Chanzo:Kisamba Media

View: https://www.instagram.com/p/Czg2ce4KoyK/
 
Apumzike Kwa Amani
Mwendo Ameumaliza
 
Dah!! Ugonjwa Mbaya sana huu... Nimeshuhudia mtu wangu wa karibu akipata shambulio la Moyo, usiombe, Dakika 1 ni nyingi kuweza kufanya chochote kujisaidia, ama kutoa taarifa ama kuomba huduma ya kwanza, hafu kadri umri unavyoenda ndo tatizo linakua kubwa...!
 
Ni kama mchezaji wa cameroun marc vivien foe alivyoanguka uwanjani kwa tatizo kama hilo. Madaktari wa timu wawe wanawapima afya wachezaji mara kwa mara kujua kama wanaweza kuhimili mikikimikiki uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…