Mchezaji wa Congo Brazzaville Aliyekatiwa Rufaa na TFF Kupimwa Leo

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Mchezaji wa Timu ya Vijana chini ya Miaka 17 Wa Congo Brazzaville anayejulikana kwa Langa Leccy Bercy na ambaye alifunga goli la Ushindi dakika za Lala Salama Dhidi Ya Serengeti Boys Pale Brazzaville,anatarajiwa kufanyiwa Vipimo Vyake Siku Ya Leo.

Mchezaji huyo alikatiwa Rufaa na TFF kwa kigezo cha kuwa na Umri Mkubwa Zaidi ya Miaka 17

Vipimo hivyo Vitafanyika Leo Nchini Misri Katika tukio hilo Tff imetakiwa kutuma daktari Wawili ili kudhibitisha majibu yatakayopatikana na pia Tff inatakiwa kulipia Gharama zote za Mchakato huo

Endapo Mchezaji huyo atabainika kweli alidanganya umri Timu Ya Serengeti boys inaweza kuingia moja kwa moja katika ushiriki wa michuano hiyo kwa kombe la Vijana Afrika chini Ya Umri wa Miaka 17 na pia Shirikisho la Soka La Congo brazzaville kupata adhabu hata ya kufungiwa kushiriki michezo hiyo

Tanzania nasisi tulishawai kukumbwa na Adhabu hiyo baada ya Zimbabwe kutukatia Rufaa dhidi ya Mchezaji wetu Nurdin Bakari(kama kumbukumbu ziko vizuri)

Tutazidi kujulishana zaidi pindi tutakapopata matokeo ya Vipimo hivyo.
 
ha ha ha ha na ikithibitika kama namuona muheshimiwa fulan atakavyopta kete ya kampeni next uchaguz
 
ha ha ha ha na ikithibitika kama namuona muheshimiwa fulan atakavyopta kete ya kampeni next uchaguz
Ila kajitaidi kwa Kiasi fulani sema Timu ya wakubwa Ndo inatuangusha

Nyasi Bandia Kaitaba,Nyamagana
Vodacom ligi Live
Ligi Ya Wanawake kuanzishwa
Ligi Ya Vijana Live

Akiweza Kutatua Shida ya Timu Ya wakubwa Atapata dole gumba kubwa sana
 
Ila kajitaidi kwa Kiasi fulani sema Timu ya wakubwa Ndo inatuangusha

Nyasi Bandia Kaitaba,Nyamagana
Vodacom ligi Live
Ligi Ya Wanawake kuanzishwa
Ligi Ya Vijana Live

Akiweza Kutatua Shida ya Timu Ya wakubwa Atapata dole gumba kubwa sana
Walitumia vigezo gain kupeleka nyas bandia kaitaba na nyamagana?naombeni kueleweshwa
 
Walitumia vigezo gain kupeleka nyas bandia kaitaba na nyamagana?naombeni kueleweshwa
Hisia zinataka kuniambia kwamba umewaza kuwa kiongozi anatoka ukanda wa ziwa ndo maana,sidhani kama ni kweli Nyamagana ilikua kwenye Mipango kuanzia kitambo sana

Na pia i think is just a distribution of resources

Next time inaweza kuwa Either Arusha,Moshi Or Kigoma
 
Utawala wa Malinzi umeitelekeza mikoa ya kisoka,eti kubalance,peleka nyasi mbeya, morogoro, kigoma etc
 
Mimi naona ingekua vyema kama wangeweka kwanza nyamagana na mwingine nyanda za juu kusini
 
Utawala wa Malinzi umeitelekeza mikoa ya kisoka,eti kubalance,peleka nyasi mbeya, morogoro, kigoma etc
Kuna kipindi Sokoine ulifungwa kwa ajili ya kupanda Nyasi za kisasa sio bandia lakini.
Sokoine una pitch nzuri tu sema matumizi ya Viwanja vyetu ni Multipurpose gwaride humohumo,mbio za mbuzi humohumo.

Cha msingi ni utunzaji wa Viwanja vyetu tuu hata hizi nyasi za kawaida zikitunzwa ni nzuri pia
 
Yule dogo nilivyomtizama! Ni kijeba Kweli, najiuliza tu wanatumia vipimo gani kutambua umri halisi wa mtu!
 
Utawala wa Malinzi umeitelekeza mikoa ya kisoka,eti kubalance,peleka nyasi mbeya, morogoro, kigoma etc
tatizo hivyo viwanja vingine ni vya chama kaitaba cha manispaa na nyamagana cha manispaa unaweza ukaweka nyasi lakini mwisho wa siku nyinyi muna mechi wao wakakuambia wana shughuri za kichama ndo maana ukawekwa nyamagana na si ccm kirumba
 
Hii timu iliniudhi sana walipocheza na Congo Dar, yaani unaongoza 3-0 nyumbani halafu unaruhusu mabao mawili 3-2?? Ile ilikuwa suicide
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…