Mchezaji wa zamani Mtibwa auawa kwa kisu akiamlia ugomvi

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986

MABULA (KULIA) AKIPAMBANA NA IDDI MOSHI WA YANGA KATIKA MICHUANO YA TUSKER KWENYE UWANJA WA TAIFA (SASA UHURU) MWAKA 2000).
Taarifa ya msiba, inaeleza beki wa zamani wa Shinyanga Shooting na Mtibwa Sugar, John Mabula amefariki dunia.
Inaelezwa Mabula aliyekuwa mtaratibu sana ameuwawa kwa kuchomwa kisu katika eneo la Kitunda jijini Dar es Salaam na muuaji wake amekimbia, sasa anasakwa na polisi.
Taarifa kutoka kwa jirani yake zinaeleza, mshambuliaji huyo amemuua Mabula ambaye alikwenda kuamua shemeji yake asishambuliwe.
Lakini baadaye akamuua na shemeji yake huyo kabla ya kumshambulia mkewe na kukimbia kusikojulikana.
Mabula alichipukia kisoka mkoani Shinyanga akiichezea Majengo kabla ya kujulikana hadi kuchukuliwa na Mtibwa Sugar aliyoichezea kwa ufanisi mkubwa.

Bado tunaendelea kufuatilia na tutawaletea taarifa zaidi.
 
Aisee Inna lillah wainna ilaih raajiun nalikumbuka hili Jina

Inatakiwa tupate mafunzo kupitia kuamua ugomvi wenye matumizi ya silaha!
 
Duuuuuuuu watu tumekuwa zaid ya wanyama kuuana kila siku
 
sisi waafrica siku zote ni makatili,hatuna huruma kama walivyo watu weupe. Sijui ni kwanini jamani..hebu tubadilikeni
 
Laani ukatili lakini usiwapambe weupe kama mfano wa wenye huruma. Mandela Patrice Lumumba Huruma wa Libya Ukraine Afghanistan Iraki Syria Yemen nk hawatatuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…