Mchezaji wa zamani wa Simba afariki Dunia

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mchezaji wa Zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia baada ya kuugua kwa kipindi kirefu jijini Dar es Salaam.

Kutoka na taarifa hizo, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe huo kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji huyo ambapo msiba wake unafanyikia Kigamboni.

"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba Arthur Mambeta ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza beki", amesema Manara.

Uongozi wa EATV kwa pamoja unawapa pole wadau wa soka nchini, familia ya marehemu na klabu ya Simba kwa kuondokewa na mtu muhimu.




Chanzo: EATV
 
TANZIA: NYOTA WA ZAMANI WA SIMBA SC AFARIKI DUNIANI
March 1, 2018 by Global Publishers

MCHEZAJI nyota wa zamani wa Simba, Urther Mambeta amefariki dunia jana jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mambeta alikuwa mmoja wa wachezaji wa Klabu ya Sunderland kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa Simba Sc kutokana na agizo la Serikali ya Tanganyika wakati huo kusisitiza timu kutumia majina ya Kiswahili.

Mambeta alikuwa mmoja wa wachezaji walioanza kuichezea Simba mwanzoni kabisa na taarifa zimeeleza msiba wake utakuwa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyezi Mungu Amrehemu.
 
kwa hiyo Simba kuifunga Yanga ni issue kubwa sana?RIP Marehemu ulietoka kustaafu na kuja kuisaidia Matopeni kuifunga Yanga ya Kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…