Mchezo wa Biko ukimaliza miezi sita, mie najitoa JF

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
8,658
Reaction score
15,793
Mchezo uliopamba moto hivi sasa wa bahati nasibu ya Biko ukimaliza miezi sita kuanzia sasa mimi najitoa JF!
Ninatabiri kuwa in the next coming six month, mchezo huu utakuwa umeshakufa kibudu.
Huu ni mchezo wa matumaini. Yani watu wengi huchangia mtu mmoja ashide.
Pale watu wanapokuwa wanacheza huku hawashindi, say kwa mara kumi, huanza kujitoa mmoja mmoja na baada ya mda kama kulikuwa kuna wachangiaji elfu kumi, mara wataanza kupungua na kubaki elfu tisa, elfu nane, elfu saba, elfu sita, elfu tano, elfu nne, elfu tatu, elfu mbili, elfu moja, and guess what, from there mchezo utacollapse.

Kama una ndoto za kucheza, ni bora ucheze sasa huenda ukashinda na kutimiza ndoto zako, ila maono yangu ni kuwa in the next six month tutakuwa tunasema R.I.P kwa mchezo huu, mchezo wa matumaini!
 
Mengi alikuwa na Jack Port Bingo, akawaweka warembo wa enzi hizo Janet Sostenes Mwenda, Hamida na yule aliyeopolewa na mzungu. Akapiga hela kisha akasepa
 
Hahaa mi na dedicate kwa hawa TATUMZUKA aisee ni wahuni wa hatari ,, huwa najiuliza sana hivi...

1.kwann kila nshindi anatoka dsm na pwani mara chache sana mbeya.

2. Wachezaji wa mikoani wana nn mpaka washinde wa dar na pwani tu.

3. Naomba kumfahamu mmiliki wa huu mchezo wa tatu mzuka. Ni namna gan huu mchezo unaendeshwa, hope ni ngumu bt namba za uxhindi unakuta wanazifaham fika so ni bosheni tu kuwachezesha watu ili wawachangie washindi wao.

4. Kwann hii michezo kipindi cha nyuma haikuwepo,

5. Je ni kweli kuwa hii michezo imeibuka kutokana hali ngumu ya maisha iliyosababishwa na mh magu.

6. In my opinion huu mchezo, na viongoz wake wote na njaa zao ni wezi tu.

7. Kwa jinsi nilivyokaa nija tathmini na kuangalia mwenendo mzima wa washindi, kwanza wanapeana kwa kujuana,
Pili, rushwa imeshamili kwenye huu mchezo,
Tatu, mtu wa mikoani akishinda wanaogopa gharama za kumpelekea mzigo wake hivyo wanampatia mtu wa dar ama pwan ili iwe rahis kumpata kwa mahtaji yao either ya ..... Wanajua wao n.k


Kama viongoz wa huu mchezo wamo humu wajiangalie,

Mambo wanayofanya sio na ni upuuzi usio na tija.

Kama masikini, ni masikini tu, kamwe huwezi kutajirikia migongo ya wanaume na wanawake wenzenu,

Pigeni kazi wizi hauna manufaa nwisho ni kufilisika na kubaki macho mnekodoa kaa mjusi kabwanwa na mlango.

Totally i hate u and if possible i pray for to get a hell far from this country.
Leo kwangu kesho kwako, watoto wenu watapata shida baadae endeleeni kuchimba shimbo msilo na ubavu wa kulifukia....


In ur your totality you are
Very big parasites ever happen.
Wezi wakubwa ninyi.
 
Michezo yote ya upatu niyakiuni tu nashangaa mpaka wakuu wa mikoa na wilaya heti wanashirikishwa kwenye ushindi wa mtu. Badala wahimize watu wafanye kazi !!
 
hivi hii michezo mbona imekuwa mingi kipindi cha magufuli
 
Jamani biko na tatu mzuka si ni utapeli huu? Daaah mpaka nakuja kubumbuluka nimesha tepeteshwaaa saaana ila roho inaniuma pesa zangu
 
Ogopa kamali ya kuchezeshwa na kompyuta.
 
Michezo yote ya upatu niyakiuni tu nashangaa mpaka wakuu wa mikoa na wilaya heti wanashirikishwa kwenye ushindi wa mtu. Badala wahimize watu wafanye kazi !!
Ata mi nashangaa mkuu ni afadhali hawa viongozi wa kiserikali wangekaa tu pembeni.
 
ivi mnatumwa mcheze? wenzenu wanalipa kodi mjue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…