Kinachonishangaza kwenye BIKO ni hivi vifuatavyo
[HASHTAG]#Kwanza[/HASHTAG] Washindi walio wengi wanatokea Dar haswa Mbagala na Tabata.
[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG] Namba zinatembea mda mchache sana. Katika kuchezesha.
[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG] Kila namba inayoshinda ikipigwa simu inapatikana muda huo huo hakuna cha network kusumbua wala nini. Haijawahi kukosekana hewani hata siku moja. Wahusika huwa hawakai mbali na simu
[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG] Nakumbuka Vodacom walikuwa wanafanyaga zao kipindi cha nyuma wakipiga haipatikani inatafutwa ya pili hadi ya tatu mbona hawa hakunaga hivyo? Au hii ni bahati nasibu ya vipi?
Ps. Kuna mchezo mchafu unachezwa nyuma ya pazia kama Tatu Mzuka tu mana hawa nao ukiweka namba kubwa wanakwambia iliyoshinda ni ndogo ukiweka ndogo wanakwambia iliyoshinda ni kubwa huu nautafsiri kama ni uhuni huu.