Kwani ninyi hamkuwahi kuiangalia ile mieleka ya akina
Power Bernado
Power Mwanza
Power Vuru Mroma
Power Chaka, nk.
Walivyokuwa wanacheza mieleka wakati ule ?
Katika WWE kuna baadhi ya matukio ya kutangaza pambano huwa wanaigiza ili kuchochea pambano.
Lakina unapoona Mkanda umewekwa ujue ni pambano halisi.
Mfano Mchezaji Jeff harry alikuwa anakataa kucheza na mdogo wake Joe harry, mdhamini alimpa pesa Joe ili amchokoza Jeff ili apandwe na hasira hadi akubali kucheza naye, hapo sasa utaona maigizo ya kuwafanya mashabiki waje kwa wingi kuuona mchezo wao.
Wazungu hawawezi kutoa pesa yao kuangalia maigizo ya mieleka.
Kama ni maigizo basi ungeona kila mtu anaicheza huo mchezo, na hata vimbaumbau wangewapiga wenye nguvu kama The Undeteka.
Kuna wachezaji wengi tu walijeruhiwa na wengine kufia uringoni.
Wakati ule wa akina Power Bernado walikuwa wanacheza kama leo unavyoona katika WWE. viti maalum vilitumika kupigania uringoni.
Mzee wangu alikuwa anapenda sana kuangalia mieleka na alikuwa anaenda na mimi karibu kila pambano la mieleka.
WWE ni mchezo halisi, na uliwahi kuchezwa hata hapa TZ.
Kwasasa mchezo huu hauchezwi hapa kwetu kwakuwa chama cha mieleka kimeshindwa kutimiza kanuni za mchezo, na kughalamia maandalizi, vifaa, matibabu, ukumbi na uringo wa mchezo huo.