Mchezo wa mieleka Una ukweli wowote?

bway hermit

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2017
Posts
1,337
Reaction score
2,339
Mchezo wa mieleka Una ukweli wowote?
Wengine wanadai ni kweli Na wengine wakidai ni mchezo unaopangwa yaani wa kuigiza tu mbele ya hadhira!!

Wapi ni wapi[emoji21][emoji21][emoji21][emoji21][emoji21]!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili lilinikanganya sana nilikutana na dada mmoja wa USA aliniambia kama ifuatavyo "WWE not really but TNA yes" kwa hiyo aliendelea kuwa WWE inakuwa sio ya kweli na wengi wanpoingia ukumbini wanakuwa washajua majibu wengine wanakuwa bado hawajajua ndo kusema katika hilo kundi ambalo hawajajua wanakuwa kama wanaangalia live. Ila TNA anasema kuwa huwa inakuwa live hayo ni majibu yake. Bado siwezi kubaki upande wake maana inawezekana ikawa sio kweli.
 
Hivi maigizo hadi kutoana damu live, au hujawahi kuangalia WWE NO MERCY?!!

sent from my Samsung smart tv using JamiiForums
 
MMA tu ndo halisi.wale jamaa wa WWE wanaitwa 'performers' so wanatufanyia maigizo tu pale.
 
maigizo.....strawman.....anamuumiza reigns hivo......duh....
 
Kwani ninyi hamkuwahi kuiangalia ile mieleka ya akina
Power Bernado
Power Mwanza
Power Vuru Mroma
Power Chaka, nk.
Walivyokuwa wanacheza mieleka wakati ule ?
Katika WWE kuna baadhi ya matukio ya kutangaza pambano huwa wanaigiza ili kuchochea pambano.
Lakina unapoona Mkanda umewekwa ujue ni pambano halisi.
Mfano Mchezaji Jeff harry alikuwa anakataa kucheza na mdogo wake Joe harry, mdhamini alimpa pesa Joe ili amchokoza Jeff ili apandwe na hasira hadi akubali kucheza naye, hapo sasa utaona maigizo ya kuwafanya mashabiki waje kwa wingi kuuona mchezo wao.
Wazungu hawawezi kutoa pesa yao kuangalia maigizo ya mieleka.
Kama ni maigizo basi ungeona kila mtu anaicheza huo mchezo, na hata vimbaumbau wangewapiga wenye nguvu kama The Undeteka.
Kuna wachezaji wengi tu walijeruhiwa na wengine kufia uringoni.
Wakati ule wa akina Power Bernado walikuwa wanacheza kama leo unavyoona katika WWE. viti maalum vilitumika kupigania uringoni.
Mzee wangu alikuwa anapenda sana kuangalia mieleka na alikuwa anaenda na mimi karibu kila pambano la mieleka.
WWE ni mchezo halisi, na uliwahi kuchezwa hata hapa TZ.
Kwasasa mchezo huu hauchezwi hapa kwetu kwakuwa chama cha mieleka kimeshindwa kutimiza kanuni za mchezo, na kughalamia maandalizi, vifaa, matibabu, ukumbi na uringo wa mchezo huo.
 
Mieleka ya WWE ni real na ndiyo mieleka bora zaidi hapa duniani
Wacheza mieleka hua trained kwa muda mrefu sana kabla ya kua drafted kwenye WWE, hii huwawezesha kucheza ule mchezo kwa ustadi mkubwa pasipo kutokea madhara hatarishi
Zifuatazo ni baadhi ya sheria muongozo kwa mchezo wa mieleka:
1. Hakuna kutumia kipepsi(elbow) kumpiga mwenzio. Hua wanatumia nyama iliyopo upande wa nyuma ya mkono kutoka kwenye kipepsi kwenda kwapani. Refer Shawn Michaels anavyomrukia mpinzani wake kutoka top cornered rope.
2. Hakuna kutumia knuckles unapompiga ngumi mwenzio.
3. Hakuna kumpiga kifuti au goti(knee) mwenzio. Kinachotumika ni nyama ya juu ya paja. Refer Brock Lesnar
4.Ngumi ya kata funua(upper cut) hairuhusiwi. Kunja vidole vyako vya mkononi vikate kiganja chako nusu ndipo unaweza piga upper cut. Refer Roman Reigns and Kane
5. Hakuna kumpiga kichwa mwenzio eneo la kati ya chini ya fore head mpaka kidevuni. Eneo lote la mdomo na pua hubaki safe
6. Hairuhusiwi kumpiga mwenzio na teke la kwenda juu na kumpiga mpinzani wako maeneo ya kidevuni akiwa ameinama au amechuchumaa. Hii huwalinda na ung'okaji wa meno

Zipo sheria nyingi zaidi zinazofanya huo mchezo uwe safe, na ukweli ni kua hakuna burudani tamu zaidi hapa duniani zaidi ya mieleka.
 

Mkuu ulimaanisha Jeff Hardy na Mart Hardy? Hawa nadhani ni twins..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…