Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikifuatilia soka la hapa bongo,ni kama lina kanuni zake tofauti na kanuni za FIFA.
Imekuwa kitu cha kawaida na hata kwa waamuzi kudhani kwa kuwa ngozi nyeusi inaonesha ugumu au usugu fulani dhidi ya mazingira ya jua,basi ni ishara kuwa watu weusi wana nguvu.Hivyo uwanjani mchezaji akichezewa faulo eneo la kumi na nane,hadi aumie sana ndipo inakuwa penalty.
Yaani kwa mujibu wa hisia za hawa watanzania wakiwemo wachambuzi wa soka,ikibidi mchezaji avunjwe miguu ndani ya box ndipo pigo la penalty liamuriwe.
Inashangaza kidogo kusikia wakisema magoli ya penalty yana hadhi ndogo kwa kuwa hawakuona kadenge na mpira kashuti goo!
Kanuni zinasema timu mgeni ifanye mazoezi katika uwanja wa mwenyeji muda ule ule mechi itakapochezwa.
Kuna maana ya kuweka kanuni hii.Wamekaa wataalamu wabobevu wa soka wakaiweka kanuni hii ikiwa na maana sana.
Wanakuja waluga luga ambao hawaamini katika kanuni za soka wanasema hamtakiwi kufanya mazoezi humu kwani kipi msichojua kuhusu uwanja huu!
Hayo ni maajabu sana,kwani timu inayocheza,wachezaji hubadilika mara kwa mara,na huenda wapo wachezaji watahitaji kujua uwanja unakuwaje.
Ninaamini soka likiachwa lichezwe kwa kanuni,kuna timu zitadondoka na kutostahili kuwa hapo zilipo,ingawa kipimo cha ukweli huwa ni mechi za kimataifa.
Huko kanuni hufuatwa na ndio maana timu kama haiko sawa ,haiwezi kufika popote.
Tubaki tu hapa kwetu tukiwa na sheria na kanuni zetu wenyewe,kama za mechi za ndondo huku tukiwaza ushirikina na tunatumia pesa nyingi kusajili.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app